Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Kiranyi wilayani Arumeru Mkoani Arusha wamefunga Barabara kwa saa kadhaa kwa mawe na Magogo wakiishinikisha serikali kuikarabati.
Barabara hiyo ya kuanzia eneo la Silent Inn kuelekea Kiranyi na Viunga vyake imefungwa na wanachi hao wakidai ilimwagwa vifusi wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa ila mpaka leo Februari 19, 2025 havikuwa vimesambazwa na kushindiliwa hali ambao ilikuwa inawapa tabu watumiaji wake.