LGE2024 Wananchi Buguruni, Njombe waomba viongozi watakao chaguliwa kukabiliana na vibaka

LGE2024 Wananchi Buguruni, Njombe waomba viongozi watakao chaguliwa kukabiliana na vibaka

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wananchi wa Mtaa wa Buguruni Kata ya Njombe mjini Mkoani Njombe wamelalamikia uwepo wa vibaka ambao wamekuwa tishio katika usalama wao na kuwataka viongozi watakaoshinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwenda kuweka mkakati wa kupambana nao.
1732260992738.png
Wananchi hao akiwemo Anna Msigwa na Maneno Ilomo wametoa Kauli Hiyo Katika Mkutano wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wakati Mgombea wa Chama cha mapinduzi CCM na wajumbe wake wakinadi sera zao na kwamba vibaka wamekuwa kikwazo kikubwa kwao.
1732260981152.png
Akinadi Sera zake kwa wananchi hao Mgombea Uenyekiti Mtaa wa Buguruni Hekima Mhagama amesema suala la Ulinzi na Usalama katika mtaa huo ni kipaumbele cha Kwanza kwake na hivyo atakwenda kukutana na vijana kuweka mkakati wa pamoja wa kukabiliana nalo endapo watamchagua.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Erasto Mpete wakati akizindua Kampeni Hizo amesema serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeendelea kutekeleza miradi mingi ya mabilioni ya Fedha na kwamba vyama vya Upinzani vinapaswa kuendelea kuwakumbusha pale wanaposahau kutekeleza.
1732261002998.png
Aidha Mpete ambaye ni Diwani wa Kata ya Utalingolo amesema katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita Kata ya Njombe mjini Imetekelezwa miradi ya zaidi ya Shilingi bilioni mbili na Hivyo endapo wananchi watawachagua wenyeviti na wajumbe wa CCM Itakuwa rahisi kuendelea kupata fedha nyingine za kutekeleza miradi mingine.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Alatanga Nyagawa amesema Tayari serikali ya Chama cha Mapinduzi CCM Inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo mengi na hivyo ili mambo yaendelee vyema ni muhimu kukipa kura chama cha mapinduzi ili kukamilisha kazi.
 
Back
Top Bottom