Wananchi Cameroon waandamana na kuchoma Majengo ya Serikali wakidai hawamtaki Rais Paul Biya

Wananchi Cameroon waandamana na kuchoma Majengo ya Serikali wakidai hawamtaki Rais Paul Biya

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Usiku wa Oktoba 15, 2025 ghasia kubwa ilizuka nchini Cameroon kufuatia maandamano ya wananchi wakichoma baadhi ya majengo ya Serikali na Jengo la chama cha Cameroon People's Democratic Movement(CPDM) kwa madai ya udanganyifu katika uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 12, 2025 huku matokeo rasmi yakiwa bado hayajatangazwa.

Wananchi wengi wamejitokeza barabarani wakipinga kile wanachokiita “uchaguzi wa wizi” na wakitaka Rais Paul Biya aondoke madarakani, wakimtaka Issa Tchiroma Bakari kutangazwa mshindi halali


1760703313689.jpeg




Katika mji wa Dschang, hali ya taharuki baada ya waandamanaji kuchoma matairi barabarani na kupaza sauti wakisema "Biya si rais wetu tena!

Taarifa zinasema kuwa jengo la chama tawala, Cameroon People's Democratic Movement(CPDM), limechomwa moto, na moshi wa mabomu ya machozi umejaza anga baada ya polisi na jeshi kuingilia kati kutawanya waandamanaji






Baadaye, waandamanaji waliendelea kulenga majengo ya serikali, ambapo mahakama ya Dschang nayo imechomwa moto


a​

Milio ya risasi na kelele za hasira zimekuwa zikirindima mitaani huku wanajeshi wakijaribu kudhibiti hali ya usalama. Mmoja wa wanajeshi waliokuwa eneo la tukio amesema wamefanikiwa kuwakamata baadhi ya washukiwa lakini bado hawajawakamata wote waliokuwa wakihusika

Tumewakamata wachache, lakini bado kuna wengine tumewakosa, ” alisema mwanajeshi huyo





Wachambuzi wanasema mvutano huu unaweza kuongezeka iwapo tume ya uchaguzi haitatangaza matokeo kwa uwazi. Wananchi wanaonekana kuchoshwa na uongozi wa muda mrefu wa Rais Biya, ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miongo minne

Kwa sasa, hali ya Cameroon inazidi kuwa tete, huku dunia ikisubiri kwa wasiwasi kuona kitakachotokea katika siku chache zijazo

Source: Karawa Media
 
Wacameroon nao walikuwa makondoo tu tena kuliko sisi, ila leo hii wamethubutu na wako kwenye uelekeo mzuri wa kumng'oa dikteta Biya..

Hii inaleta matumaini kwakweli kuwa afrika nzima sasa inaelekea kukombolewa.
 
Ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2025-2030 imetamka wazi kuwa itafanikisha mchakato wa katiba mpya.
Ninawasihi tuwe na subira viongozi wetu wafanye kazi kwa utulivu ili watuletee maendeleo.
#Tanzania kwanza.
Haya mambo ya Tz yanaingia vipi? Mada ni ya yanayoendelea Cameroon, au umerogwa?
 
Kwahyo hakuna Comment iliyotaja TZ zaidi ya hiyo tu??
Au wewe ndio umerogwa🤔
 
Ccm tujifunze katika haya yanayopata wenzetu.

Waswahili walisema kiburi sio uungwana.

TUJISAHIHISHE KELELE ZIMEKUWA NYINGI SANA HAZIPASWI KUPUUZWA.
 
Ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2025-2030 imetamka wazi kuwa itafanikisha mchakato wa katiba mpya.
Ninawasihi tuwe na subira viongozi wetu wafanye kazi kwa utulivu ili watuletee maendeleo.
#Tanzania kwanza.
Kikwete alikuja na huu utapeli akatuacha na rasimu.
Hatudanganyiki..!! Tukutane 29/10
 
Mm nataka viwanja na maeneo yote yanayomilikiwa na chama tawala yachukulie km yawe chini ya NHC...yaaan yoote nao wakapange ...yaan ni kuwavuruga mpaka nao waone cha moto
 
Usiku wa Oktoba 15, 2025 ghasia kubwa ilizuka nchini Cameroon kufuatia maandamano ya wananchi wakichoma baadhi ya majengo ya Serikali na Jengo la chama cha Cameroon People's Democratic Movement(CPDM) kwa madai ya udanganyifu katika uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 12, 2025 huku matokeo rasmi yakiwa bado hayajatangazwa. Wananchi wengi wamejitokeza barabarani wakipinga kile wanachokiita “uchaguzi wa wizi” na wakitaka Rais Paul Biya aondoke madarakani, wakimtaka Issa Tchiroma Bakari kutangazwa mshindi halali



Katika mji wa Dschang, hali ya taharuki baada ya waandamanaji kuchoma matairi barabarani na kupaza sauti wakisema "Biya si rais wetu tena!

Taarifa zinasema kuwa jengo la chama tawala, Cameroon People's Democratic Movement(CPDM), limechomwa moto, na moshi wa mabomu ya machozi umejaza anga baada ya polisi na jeshi kuingilia kati kutawanya waandamanaji


Baadaye, waandamanaji waliendelea kulenga majengo ya serikali, ambapo mahakama ya Dschang nayo imechomwa moto



Milio ya risasi na kelele za hasira zimekuwa zikirindima mitaani huku wanajeshi wakijaribu kudhibiti hali ya usalama. Mmoja wa wanajeshi waliokuwa eneo la tukio amesema wamefanikiwa kuwakamata baadhi ya washukiwa lakini bado hawajawakamata wote waliokuwa wakihusika

Tumewakamata wachache, lakini bado kuna wengine tumewakosa, ” alisema mwanajeshi huyo





Wachambuzi wanasema mvutano huu unaweza kuongezeka iwapo tume ya uchaguzi haitatangaza matokeo kwa uwazi. Wananchi wanaonekana kuchoshwa na uongozi wa muda mrefu wa Rais Biya, ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miongo minne

Kwa sasa, hali ya Cameroon inazidi kuwa tete, huku dunia ikisubiri kwa wasiwasi kuona kitakachotokea katika siku chache zijazo

Source: Karawa Media
Yes,prophecy fulfilled....hayati alisema haya,5 yrs now na itatembea nchi kwa nchi....
More to come
Tunzeni pesa zenu
 
Back
Top Bottom