Hali ya wasiwasi imekithiri katika miji mbalimbali ya Cameroon, kufuatia madai ya ushindi yaliyotolewa na mgombea wa upinzani, Issa Tchiroma Bakary, katika uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 12, 2025
Soma Kiongozi wa Upinzani ajitangaza Mshindi wa Urais Cameroon, amuomba Rais Paul Biya akubali Matokeo
Wakazi wa Jiji la Maroua, makao makuu ya Mkoa wa Kaskazini Mashariki mwa Cameroon wameshikwa na msisimko mkubwa huku wakiapa kulinda kile wanachokiona kama ushindi halali usiopingika. Wafuasi wa chama cha FSNC, wakiamini kuwa mgombea wao alipata kura nyingi zaidi, wamemiminika mitaani kwa wingi wakiwa chini ya uongozi wa Mratibu wa Kanda, Ibrahim Bouba. Wanasema wako tayari kusubiri ishara rasmi kutoka kwa “rais” wao kabla ya kuanza kusherehekea
Morali iko juu, na matumaini yamejaa tele. Wananchi wanadai kuwa wanayo nakala rasmi za matokeo kutoka vituo vya kupigia kura katika maeneo mbalimbali ya kanda hiyo, zikionyesha wazi kuwa Issa Tchiroma Bakary ndiye mshindi halali wa uchaguzi. Uhakika huo umewapa ari isiyotetereka ya kulinda matokeo
Ujumbe kutoka kwa wafuasi wa FSNC ni mmoja: wamejipanga kikamilifu kumpa mgombea wao uungwaji mkono wa bila masharti. Wanasisitiza kuwa hawatakubali jaribio lolote la kupindua matokeo ya kura wakitaka kuona sauti yao inaheshimiwa
Wakati hali ikiendelea kuwa tete Maroua, mvutano umeenea pia katika mji wa kibiashara wa Douala, hasa katika eneo la Santa Barbara, ambako kumekuwa na makabiliano kati ya raia na askari wenye sare. Wananchi wanataka ukweli kuhusu matokeo ya uchaguzi huo
Kwa mujibu wa duru za kisiasa, Rais Paul Biya ambaye ametawala Cameroon tangu mwaka 1982 — amepoteza uchaguzi huo, na anadaiwa kujaribu kwa siku kadhaa kuchezea matokeo, hatua ambayo imezidisha hasira za wananchi na kuhatarisha utulivu wa taifa
Cameroon sasa iko katika kipindi cha wasiwasi mkubwa, huku dunia ikifuatilia kwa makini mustakabali wa taifa hilo la Afrika ya Kati
Waandamanaji jijini Douala wameanza kubomoa mabango na picha za Rais Biya, wakitoa wito kwa serikali kuheshimu matokeo ya kura na kumruhusu mshindi halali kuchukua hatamu za uongozi