Wananchi Hai, Simanjiro na Arumeru wafunga barabara kwa saa nne waitaka Serikali kutatua changamoto

Wananchi Hai, Simanjiro na Arumeru wafunga barabara kwa saa nne waitaka Serikali kutatua changamoto

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wananchi wa Kata ya Kia (Wilaya ya Hai, Kilimanjaro), Majengo (wilayani Arumeru, Arusha), na Naisinyai (wilayani Simanjiro, Manyara) wameandamana na kufunga barabara ya Mirerani hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), wakishinikiza Serikali kutatua changamoto ya eneo korofi linalosababisha mafuriko ya mara kwa mara katika maeneo yao.

Wananchi hao wamesema mafuriko katika mpaka wa Kata za Majengo, Naisinyai, na Kia yamesababisha vifo na uharibifu wa mazao ya chakula, hivyo maandamano yao yamelenga kutoa ujumbe wa amani kwa mamlaka husika.

Maandamano hayo yalifanyika leo, Jumanne Februari 11, 2025, ambapo barabara hiyo ilifungwa kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa 2:44 asubuhi. Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Amir Mkalipa, alifika eneo hilo na kuzungumza na wananchi, akiwaomba kufungua barabara ili kuruhusu abiria waliokwama kuendelea na safari zao.

Aidha, DC Mkalipa aliwahakikishia wananchi kuwa kesho kutafanyika kikao cha pamoja kati ya wakuu wa wilaya hizo tatu, madiwani, pamoja na wenyeviti wa vijiji husika kwa lengo la kujadiliana na Bonde la Pangani kuhusu utatuzi wa tatizo hilo.

Snapinst.app_478140252_18460061593065701_3461573905435476359_n_1080.jpg
 
Hawajakamatwa kweli
Case za hivi wakikamatwa wenzao wanawavaa viongozi wao,inageuka siasa lazima watafute njia watolewe na kesi ifutwe..viongozi wanaotegemea kupigiwa kura ndo wahanga
 
Back
Top Bottom