Halafu mkiambiwa kuwa Magufuli alikuwa Rais mzuri sana na asiyependa watendaji wababaishaji NYIE HAMTAKI. NINAAMINI ANGEKUWEPO LEO HIZO BARABARA ZINGESHAWEKWA LAMI TENA SIO LAMI YA UBABAISHAJI .Magufuli aliiweka hiyo barabara ya Msumi katika mpango wa TANROAD ...ilitakiwa iwekwe lami kitambo kama wenzenu wa barabara ya Mbezi -Goba walivyowekewa lami na Tegeta-Madale-Goba njia nne walivyowekewa lami.
Maendeleo yanachelewa kuja msumi kutokana na ubovu wa barabara. GOBA sasa hivi viwanja havishikiki kutokana na maendeleo ya barabara na huduma nyingine za kijamii kuwa karibu na wananchi.
Mawaziri na watendaji wa serikali kipindi cha Magufuli walikuwa wanawajibika kwa lazima sababu ya yule mwamba. LEO HII WAMEGUNDUA MAMA YETU NI MPOLE BASI WANAFANYA WANAVYOTAKA. NA NINAAMINI MAMA ASIPOIULIZIA HIYO BARABARA BASI MJUE ITAFIKA MWAKA 2030 IPO HIVYOHIVYO.
TUMIENI KIPINDI HIKI CHA NWEZI WA RAMADHAN NA KWARESMA KUMUOMBA MUNGU ILI MAMA YETU ASIKIE KERO HIZO ZA BARABARA HALAFU ATOE MAAGIZO. MAANA JAMAA BILA MAAGIZO HAWAFANYI. WATAKACHOFANYA NI UBABAISHAJI WA KUWALETEA GARI LA KUCHONGA BARABARA HALAFU NDIO IMETOKA HIYO.
NA MSUMI KULIVYOJIFICHA HUKO HAKIKA WADAU WA SERIKALI NDIO WANAFURAHI MAANA SIO RAHISI VIONGOZI KUIONA HIYO BARABARA.