Wananchi hatuna mashaka na Rais wetu Samia mpaka sasa, nchi imefunguka

Fukua

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2022
Posts
546
Reaction score
479
Nawasalimu woote Kwa jina la JMT

Moja Kwa Moja KWENYE mada

Mauzo ya bidhaa zetu nje ya nchi yameongezeka sana.

Kilio Cha tozo serikali imekisikia na Sasa tuna Ari ya kuchangia maendeleo yetu maana hayupo wa kufanya Kwa ajili yetu. Demokrasia Na utawala Bora nchini Sasa sawa kabisa na Marekani.

Uhuru wa vyombo vya habari ni WA kutosha kabisa sote ni mashahidi. Furaha mioyoni mwa wananchi ni KUBWA sana,mataifa yote ya Dunia yamekuwa na Imani na Tanzania, wawekezaji na watalii wanamiminika,

Miradi mikubwa inaendelea kujengwa,chama chetu cha CCM kinapendwa na wananchi haijawahi kutokea, Kwa hiyo ushindi 2025 si wa mashaka hata kidogo.

Wapinzani NAO wanaona aibu hawana agenda KUBWA au ya msingi ya kukosoa serikali wananchi wamewapuuza.

Ufisadi na rushwa vimepungua sana. n.k n.k. Nchi iko salama salimin. Kiukweli mama, wananchi wanakupenda, wanakuheshimu na wanakuombea Kwa Mungu uwe na AFYA njema utuvushe salama.

Vyombo vya ulinzi na usalama vipo imara
Baraza lako la mawaziri liko safi.
Bunge liko makini
Mahakama iko poa
Wananchi WAKO Tuko safi tumedhirika tunachapa kazi, tunakuunga mkono hatuna wasiwasi na utendaji wako.

Mambo mazuri ni mengi siwezi kuyamaliza Kwa kuyataja hapa.itoshe TU kusema una upiga mwingi.

Kidogo kinachotia ukakasi ni haya matusi ya wapinzani wachache huku mitandaoni, lkn tutawapuuza kama ulivyofanya wewe kiongozi wetu mama shujaa wa Karne hii.

Watanzania Tunajivunia kupata kiongozi safi na makini endelea KUIFUNGUA NCHI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…