Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Ismail Mwakiagi, Shaban Ngomoli na Johari Tito wamesema kodi ya ardhi na kodi ya jengo zimekua zikiwachangana ambapo wameiomba serikali kufuta kodi mojawapo ili kupunguza mzigo mkubwa kwa wananchi.
Kamishina msaidizi wa ardhi mkoa wa Katavi Chidiel Mrutu amesema kodi ya ardhi inapaswa ilipwe kila mwaka ambapo ifikapo juni 30 kuhakikisha kila mdaiwa analipa kodi hiyo huku akidai kupelekwa katika vyombo vya sheria kwa yeyote atakaye kaidi.
Mrutu amesisitiza kila mdaiwa kuhakikisha analipa kodi hiyo katika ofisi za ardhi ili kuongeza pato la serikali kwa maslahi ya Taifa.