Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana jana Dodoma, chini ya Mwenyekiti wake Samia Suluhu, imeiagiza Serikali kuchunguza mwenendo wa Jeshi la Polisi baada ya wananchi kupoteza imani na Jeshi hilo.
Inadaiwa Maofisa wa Polisi hawaaminiki na wanaonekana kutenda majukumu yao bila kufuata Mwongozo wao wa kisheria (PGO).
Shaka Hamdu Shaka amezungumza hayo alipokuwa anaongea na Waandishi wa Habari kuhusu kikao hicho cha CCM kilichofanyika jana.
Akiongea na waandishi leo Machi 12, 2022, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema ‘’Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa imeielekeza Serikali kuangalia upya mwenendo wa Jeshi la Polisi nchini ambao umekuwa hauridhishi na kulalamikiwa na wananchi kutokana na matendo yanayofanywa na baadhi ya maofisa na askari wa Jeshi hilo kinyume na muongozo wa kazi za Jeshi la Polisi"