Wananchi kukosa imani na Polisi: CCM yaagiza Jeshi la Polisi lichunguzwe

Polisi hawazi kupendwa na mwananchi hata siku moja tangu enzi za yesu na kabla ya yesu askari hakuwahi kupendwa kwa kilichopo polisi akitenda majikumu yake ipasavyo tayari mwananchi atamuona ni mtu mbaya,jambo la msingi mwananchi afuate sheria na kutii mamlaka zilizopo hakuna kingine hata jeshi libadilishwe vp sijui lakini kama halitakabiliana na wahalifu itakuwa ni kazi bure.
Utakuwa mpuuzi kiwango cha Kingai kutueleza huu upuuzi. Yule kijana aliyeuawa Mtwara ulitaka atii nini ili asichomwe sindano ya sumu?
Wiki iliyopita tulimwona Waziri wa jinsia na Watoto akimsimamisha Askari wa kike na kusema amesikia sifa zake jinsi Wananchi wanavyomkubali. Ukiwa mtenda haki Wananchi watakuchukia Kwa lipi? Huu uhuni wa kudhani Wananchi wanaichukia Polisi bila sababu ya msingi ni upuuzi usiopaswa kusikilizwa na Wenye akili.

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
We shaka we! Ccm si ndio inalifanya jeshi la police kudharaulika.
Ina maana leo mnawakana ndugu zenu.
Kwa katiba hii Kazi ya police ni kulinda chama.
 
Bila katiba mpya Katu police hawawezi kuwa huru.
Kama Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya na mkoa ni ccm sasa utawatenga vipi police na ccm.
Kwani anaeamuru ocd kamata huyu weka ndani si DC au RC na hawa ni lazima uwe ccm.
 
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana jana Dodoma, chini ya Mwenyekiti wake Samia Suluhu, imeiagiza Serikali kuchunguza mwenendo wa Jeshi la Polisi baada ya wananchi kupoteza imani na Jeshi hilo.

Inadaiwa Maofisa wa Polisi hawaaminiki na wanaonekana kutenda majukumu yao bila kufuata Mwongozo wao wa kisheria (PGO).

Shaka Hamdu Shaka amezungumza hayo alipokuwa anaongea na Waandishi wa Habari kuhusu kikao hicho cha CCM kilichofanyika jana.

Akiongea na waandishi leo Machi 12, 2022, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema ‘’Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa imeielekeza Serikali kuangalia upya mwenendo wa Jeshi la Polisi nchini ambao umekuwa hauridhishi na kulalamikiwa na wananchi kutokana na matendo yanayofanywa na baadhi ya maofisa na askari wa Jeshi hilo kinyume na muongozo wa kazi za Jeshi la Polisi"
Ndio shida ss
 
Anatafutwa mtu mmoja tu hapo, ndio target.
 
Polisi hawazi kupendwa na mwananchi hata siku moja tangu enzi za yesu na kabla ya yesu askari hakuwahi kupendwa kwa kilichopo polisi akitenda majikumu yake ipasavyo tayari mwananchi atamuona ni mtu mbaya,jambo la msingi mwananchi afuate sheria na kutii mamlaka zilizopo hakuna kingine hata jeshi libadilishwe vp sijui lakini kama halitakabiliana na wahalifu itakuwa ni kazi bure.
Pale mlipomuua yule jamaa wa Mtwara mlikuwa mnatekeleza majukumu eeeh?.
 
Hapo pagumu,labda ifanyike Reform ya vikosi vya polisi.
Njia mmoja wapo ya reform ni kutumia polisi wa nchi kama Uingereza kuiunda au kuisuka upya police force ya Tanzania.
Lakini hadi CCM yenye kuongoza serikali yake imekiri na inalalamika sana basi kuna mambo mengi maovu.
Lakini nao polisi wanapewa amri tata,na hao viongozi wanasiasa.Yawezeka ubovu wa polisi umesababishwa na wanasiasa watawala.
Itakuwa sio haki ukiwaacha viongozi wa serikali kutowajibika kwa amri za kinyama.
 
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana jana Dodoma, chini ya Mwenyekiti wake Samia Suluhu, imeiagiza Serikali kuchunguza mwenendo wa Jeshi la Polisi baada ya wananchi kupoteza imani na Jeshi hilo.

Inadaiwa Maofisa wa Polisi hawaaminiki na wanaonekana kutenda majukumu yao bila kufuata Mwongozo wao wa kisheria (PGO).

Shaka Hamdu Shaka amezungumza hayo alipokuwa anaongea na Waandishi wa Habari kuhusu kikao hicho cha CCM kilichofanyika jana.

Akiongea na waandishi leo Machi 12, 2022, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema ‘’Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa imeielekeza Serikali kuangalia upya mwenendo wa Jeshi la Polisi nchini ambao umekuwa hauridhishi na kulalamikiwa na wananchi kutokana na matendo yanayofanywa na baadhi ya maofisa na askari wa Jeshi hilo kinyume na muongozo wa kazi za Jeshi la Polisi"
It is justified and too late.Jeshi la Polisi limepoteza mwelekeo kabisa.Livunjwe na liundwe upya.
 
Chama-dola nacho kinaanza kuistukia Polisi? Au CCM hawaridhishwi na kuona sasa polisi inaanza kufuata PGO
 
Kwa katiba yetu, ni mtu mmoja tu, hubadili mfumo mzima. Mkiwa na Rais katili, kila chombo cha serikali huwa katili. Mkiwa na Rais muungwana, kila chombo kinabadilika.

Rais Samia, tunakuomba ulibadilishe jeshi la polisi kutoka kwenye ukatili kwenda kqenye ustaaabu na utu. Ustaarabu ni kufuata taratibu na sheria.
KAMA ALIOFANYIWA KUBENEA, DR. ULIMBOKA, MWANGOSI N.K?
 
Kwa katiba yetu, ni mtu mmoja tu, hubadili mfumo mzima. Mkiwa na Rais katili, kila chombo cha serikali huwa katili. Mkiwa na Rais muungwana, kila chombo kinabadilika.

Rais Samia, tunakuomba ulibadilishe jeshi la polisi kutoka kwenye ukatili kwenda kqenye ustaaabu na utu. Ustaarabu ni kufuata taratibu na sheria.
Bora ungemuomba Kikwete moja kwa moja atusaidie kwa hili.
 
jeshi haliwezi kujichunguza lenyewe tusidanganyane .
yaani imefikia kipindi tunaogopa hawa wanaumwe wasiokua na ndevu kuliko jambazi

Polisi walinidhurumu laptop na simu zangu za mkononi na pesa niliyokua nayo mfukoni kama 170k hv na nilipotaka kulianzisha ili nipate vitu vyangu wakataka kunipa kesi ya kuhujumu uchumi.

ila nasema hv: ipo siku tu inakuja
 
Back
Top Bottom