Wananchi kukosa imani na Polisi: CCM yaagiza Jeshi la Polisi lichunguzwe

Je tutarajie mabadiliko kwenye jeshi hilo ?
Hao wajumbe wamesahau fadhila wanazopewa na jeshi hilo?

Au swali liwe: Wajumbe wanajisahaulisha kazi waliyowapa jeshi; kazi ya kusimamia maslahi ya chama chao?

Je, hawa wajumbe wanajua bila polisi chama chao kitakuwa matatani sana?
 
Mkuu 'Bams', (omba?) dai KATIBA mpya.
 
Ccm acheni kutufanya sisi kama watoto nyie ccm ndio tegemeo lenu ndio sanduku lenu la kura alafu leo muwachunguze thubutuuuu nyie semeni kesi ya mbowe mliombambikia imaewaozesha kila kiungo na mnataka kuwastafisha Kwa heshima siro na wenzie Kwa aibu hiyo,mnataka kuwazuga wananchi tu
 
Fumua Jeshi lote mwanzo mwisho vinginevyo ni danganya toto tu, na kufanya reforms muhimu katika ngazi zote.
 
Umemaanisha Principal amchunguze deputy principal ?
 
Kwamba kamati kuu ya ccm inayosimamiwa na SSH imeiagiza serikali inayosimamiwa na SSH kuichunguza Tanpol ambayo mkuu wake ni mteule wa SSH.

Ujinga mtupu!
Tunacheleweshana wenyewe!!

Siro na polisi wake kadhaa watawajibishwa lakini bila #Katiba_Mpya! tutarudi kwenye shimo hilo hilo.
 
shida wenyewe wanaozunguza hivyo,baadae wanataka watetewe na haohao.siasa kigeugeu
 
Tuache unafiki ipo siku haki itapatikana. Polisi ni mtaji wa ccm na ccm imeunda serikali halafu serikali iwachunguze polisi !!!, acheni kudanganya watu.
hapo hapo CCM inayoongozwa na Mwenyekiti inaiagiza serikali inayoundwa na CCM na kuongozwa na Rais ambaye ndiye huyo huyo mwenyekiti wa CCM
 
Hii ndio sababu iliyonisukuma kuleta uzi huu
 
Anatafutwa Siro hapo
Yaani hapo ndo destination hakuna kingine. Kwa sababu uongozi unataka sisi raia tuupende wanauzunguka mbuyu mpaka raia waseme. Lakini hawajuhi kwamba jeshi la polisi limeridhi tamaduni za jeshi la mkoloni na mafundisho yote yanaegemea kwenye experience ya kikoloni
 
Kuna siku nikiwa njiani mbele yetu kulikuwa na gari ya doria ikasimama katikati ya road wakawa wanasalimiana na jamaa muda mrefu na njia nyembamba haiwezekan kupita pembeni
Nikavumilia kwa dakika kadhaa nikawapigia honi wakae pemben japo gari iliyokuwa nyuma ya gari hiyo ya doria haikuwa imepiga honi…akashuka askari mmoja akagundua gari yangu ndio imepig honi…akaja akaanza kufoka Weee Mzee huoni gari gani imesimama mbele hadi unapiga honi…nikamjibu nimeona…nikaishia hapo nikajifanya kama hamnazo flani hivi akaenda kumwita incharge wake ambae alikuwa nadhan A/inspector akaniuliza Mzee una shida gani? Nikamwambia shida yangu safari yangu imekwamishwa na gari yenu na hakuna ishara yoyote kuashiria lolote hivyo siwezi kujua nigeuze gari nirudi nilipotoka au nisubiri mmetu block labda mna shida na sie or what?…jamaa akasema ukiona tumesimama sehemu na gari na gari ya Doria tambua kuna jambo la msingi ndio limetusimamisha sie hatupo matembezini kama Wewe…nikawajibu sawa sikuwahi kufahamishwa hilo kwa miaka yote japo nami nimepita mlipo nyinyi kwa miaka kadhaa lakin najua labda kuna maboresho kadhaa ya kanuni labda hiyo nyongeza sijawa updated

Kwa kifupi jamaa wale wanajiona wao ndio sheria
Ukisumbua geshi ra porisi lazima upigwe tu hakuna namna!
 
Waache kujikosha. Hilo jeshi linawatumikia wao. Wamelilea hivohivo.
 
Katiba
 

Wapuuzi sana hawa watu. Anayewapa police illegal orders ni watawala wenyewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…