Wananchi kuteleza sio kuanguka mnao uwezo mkubwa wa kubadili mambo, belouzdad wamewaamsha rasmi!

Majok majok

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2023
Posts
783
Reaction score
2,057
Naweza kusema kwenye mpira uwa Kuna siku mbaya kazini Kila kitu kinaweza kwenda tofauti na mipangilio ya siku zote, na Jana yanga walikuwa na siku mbaya kazini!
Timu ili icheze vizuri inatakiwa Kila mchezaji awe timamu kimwili na kiakili na Kila mchezaji atimize majukumu yake ipasavyo lakini kwa Jana ilikuwa ngumu kwa yanga kutokana na changamoto zilizojotokeza ambazo ni Kama ifuatavyo;
Mosi; Wachezaji wengi awakuwa timamu nafikiri kitendo Cha kukaa siku 14 bila kucheza mechi yoyote ya kiushindani imewafanya wakose match fitness ambayo wenzao walikuwa nayo kwani mpaka wanacheza Jana tiyali walikuwa wamecheza match zao za ligi 3 mfululizo na iyo tumeona kwenye uharaka wa kufika kwenye matukio muhimu uwanjani!

Pili; Wachezaji walioitwa timu za taifa kukosa maandalizi ya pamoja na wenzao pia imechangia, lakini fatique imechangia pakubwa kwa wachezaji wengi kutokuwa kwenye ubora wao, tumeona Aziz ki, mudathir, job na baka wakiwa awako sawa kwenye maamuzi yao uwanjani nafikiri uchovu umewaathiri pakubwa sana

Tatu; Eneo la goal keeping alikuwa kwenye mikono salama baada ya kukosekana kwa Djigui diara, kukosekana kwake kumeleta athari pia kwani mabeki wanapokuwa wanacheza na kipa wanayemuamini uwa wanakuwa comfortable na mpira tofauti wakiwa wanacheza na kipa ambae awamwamini, kitu icho kimeonekana Jana Metacha footwork yake sio nzuri ata kidogo, ajui ata kuanzisha mashambulizi matokeo yake alikuwa anapiga pasi nyingi mkaa isipotoka nje itaenda kwa adui, ni kitu ambacho kiliwafanya mabeki wacheze kwa kutokujiamini kabisa, djigui diara aliumia bega ndio maana alikosekana mechi ya coast na ya taifa pia akucheza!

Nafikiri hizo ni sababu kuu zilizopelekea yanga kupata matokeo hasi Algeria licha ya umiliki wa takwimu zote za kimchezo but point 3 muhimu ndio kinachotakiwa kwenye hii hatua!
Pamoja na ayo yote bado yanga wanayo nafasi kubwa ya kusonga mbele kwa uwezo wa kikosi Chao,
Bado zipo point 15 za kupigania ambazo ni muhimu na ukiangalia vizuri ratiba ilivyokaa yanga wanao uwezo wa kutinga robo fainali, watacheza mechi 3 nyumbani na mbili ugenini, kwa maana iyo wanatakiwa kuchukua point 9 za nyumbani na kutafuta SARE 2 ugenini ili wavuke, wakifanikiwa kupate matokeo kwa Aly ahly basi itakuwa ndio starting point nzuri ya kusonga mbele,
Kwenye hatua zote ambazo Simba alifanikiwa kuingia robo fainali akuwai kushinda ata mechi moja ugenini, alipata point kwenye uwanja wa mkapa lakini kwa uwezo wa yanga hii anaweza kupata matokeo ata nje ya Tanzania bila wasi wasi,
Kwenye mechi ya belouzdad yanga walifanya makosa na wakaadhibiwa, ukifanya makosa unaweza kufungwa ata goli 10 ndio maana ukaitwa mpira wa miguu utakuwa na matokeo 3,
Wake up call waliyoipata Jana itawaamsha na mechi ijayo dhidi ya Aly ahly itakuwa tofauti sana WANANCHI watarudi kwa nguvu kwenye ubora wao, nategemea mechi nzuri sana siku iyo!
 
Tutafungua nyuzi nyingi sana kuhusu mchezo wa jana. Ila ukweli hautabadilika kuwa tumeruhusu kupoteza point 3.

Kwangu naona ni matokeo ya mpira maana wahenga wanasema, one mistake one goal.

Yanga jana waliingia kwenye mfumo wa waarabu, jamaa hawakutaka kuchezea nafasi, wakatunyuka
 
Inawezekana pasina shaka wala tashwishwi yeyote
 
Nafiriki yanga iyo jana ingeshinda sidhani kama ungekuja na hoja izo za manung'uniko ulizozitaja.....Hii ni michuano ni mikubwa sana unatakiwa ukicheza ugenini kuna stail yake unayotakiwa kucheza,jana yanga wanaingia uwanjani hawakuwaheshimu wapinzani wao,walitakiwa kucheza mchezo wa kujihami sana ila wao wakaamua kufunguka
 
Mpira ni mbinu, wakati mwingine unaachwa ucheze mpira siyo kwamba unaogopwa la hasha, jamaa waliisoma yanga kitambo tu. Wakaona tundu kubwa pembeni, wakaona beki wa pembeni mmoja huyu kurudi kuzuia ni mtihani hivyo hii ni njia nzuri, halafu wakaamua kujazana katikati maana hii ni njia yanga kupiga pasi aahh basi shughuli ikaisha, waache wacheze huku sisi tukiabsorb weakness zao, yanga wanavyozidi kucheza ndivyo weakness na matobo yanavyozidi kuonekana... professional level Huwa Iko hivyo otherwise Kwa mpira wa Jana wa yanga ilihitaji wachezaji wa daraja la juu kabisa Ili kushinda.
 
Kwanini msiseme tu kwamba belzoudad ni Bora zaidi yetu
 
Kubalini uwezo uliamua matokeo. Hivi mnajua kocha wa CRB amefundisha hadi kwenye Kombe la Dunia? Wale jamaa hata hapa wanakuja kuwapiga tena.

Na kuhusu kukaa siku nyingi bila kucheza, tunapowaambiaga na kuwashangaa mnavyokwepaga mechi za ndani kwa kisingizio cha mechi za kimataifa huwa hamtuelewi. Leo ndiyo mnaelewa. Halafu wakati huo huo unasema wachezaji waliokuwa wanacheza mfululizo wamechoka. Tuchukue lipi sasa?
 
Nafiriki yanga iyo jana ingeshinda sidhani kama ungekuja na hoja izo za manung'uniko ulizozitaja.....Hii ni michuano ni mikubwa sana unatakiwa ukicheza ugenini kuna stail yake unayotakiwa kucheza,jana yanga wanaingia uwanjani hawakuwaheshimu wapinzani wao,walitakiwa kucheza mchezo wa kujihami sana ila wao wakaamua kufunguka
Mpira ni mchezo wa makosa hakuna cha ugenini au nyumbani , simba alicheza kwa mkapa na sio ugenini akala 3-0 na ugenini akala 3-1 .

Yanga alifanya makosa jana akaadhibiwa tusubiri next game huenda kocha akarekebisha makosa .

Waalgeria Kama walivyofanya Morocco WC 2022 walipaki basi nyuma wakafanya counter za uhakika na accurate passing wakamaliza mchezo.
 
Back
Top Bottom