Wananchi kuwasha moto mitaani kwenye Maandamano Ufaransa ya kutaka Rais Macron ajiuzulu

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Zaidi ya watu 200,000 wameandamana na mamia wakamatwa nchini Ufaransa Septemba 11, 2025 kufuatia maandamano makubwa ya kitaifa yaliyoanza Septemba 10, 2025 wananchi wakipinga mipango ya kupunguza bajeti na hali tete ya kisiasa nchini humo.​
1757592204594.png
Vuguvugu hilo lililopewa jina “Fungeni Kila Kitu” liligeuka kuwa mapambano makali, mitaa ikijaa moshi, vizuizi vya moto na gesi ya machozi. Hali hii imekuwa mtihani mzito kwa Rais Emmanuel Macron baada ya kumteua Waziri Mkuu mpya, Sebastien Lecornu.

Licha ya serikali kupeleka polisi 80,000 kudhibiti hali, vurugu zilisambaa kote nchini. Huko Rennes, basi liliunguzwa moto, huku nyaya za umeme zilizokatwa kusini magharibi zikisitisha huduma za treni na kusababisha msongamano mkubwa wa magari.

Waziri wa Ndani, Bruno Retailleau, alisema karibu waandamanaji 200,000 walishiriki, ingawa chama cha wafanyakazi cha CGT kilikadiria idadi hiyo kuwa zaidi ya 250,000. Kufikia jioni ya Septemba 10 polisi walikuwa wamewakamata zaidi ya watu 450, mamia wakiwa bado rumande, zaidi ya maafisa 12 walijeruhiwa, na zaidi ya matukio 800 ya maandamano yaliripotiwa kuanzia maandamano ya amani hadi moto mitaani. Retailleau alidai kuwa siku hiyo ilikuwa “ushindi dhidi ya waliotaka kufunga taifa,” lakini takwimu za serikali zilionesha hali tofauti.
​
1757592247849.png
Maandamano haya yamefufua kumbukumbu za vuguvugu la Yellow Vest mwaka 2018, na yanaonesha hali inayojirudia katika urais wa Macron: polisi wengi mitaani, ghasia, na mvutano wa kudumu kati ya wananchi na serikali.
Tangu achaguliwe tena mwaka 2022, Macron amekabiliwa na hasira kubwa ya wananchi—kuanzia mageuzi ya pensheni yaliyoibua upinzani mkali, hadi ghasia za kitaifa baada ya polisi kumuua kijana katika vitongoji vya Paris mwaka 2023.​

Maandamano ya wiki hii yamechochewa na kuanguka kwa serikali Jumatatu, baada ya Waziri Mkuu wa zamani François Bayrou kushindwa kwenye kura ya imani bungeni. Macron alimjibu kwa kumteua mshirika wake wa karibu na Waziri wa Ulinzi, Sebastien Lecornu, kuwa Waziri Mkuu mpya. Hii inamfanya Lecornu kuwa Waziri Mkuu wa tano chini ya miaka miwili na wa nne ndani ya mwaka mmoja pekee.

Sasa, kwa sauti za “Macron ajiuzulu” zimesambaa kote nchini, huku maandamano haya yakionyesha udhaifu wa uongozi wa kisiasa na hasira ya wananchi dhidi ya serikali.

===============For English Audience============​

France’s streets ablaze as antigovernment protests disrupt daily life Hundreds arrested after more than 200,000 demonstrators force French government into high-stakes confrontation. A protester displays a French national flag next to burning rubbish bins. A protester of the 'Block Everything' movement displays a French national flag next to burning rubbish bins in Lille, northern France.

A nationwide wave of antigovernment protests swept across France, filling streets with smoke, burning barricades and tear gas as demonstrators rallied against budget cuts and political instability. The “Block Everything” campaign created a formidable test for President Emmanuel Macron and transformed Sebastien Lecornu’s first day as prime minister into an immediate crisis. While the movement did not achieve its goal of total national disruption on Wednesday, it successfully paralysed significant portions of daily life and ignited hundreds of flashpoints throughout the country.

Despite deploying 80,000 police officers who dismantled barricades and arrested hundreds, disturbances multiplied across France. Protesters torched a bus in Rennes, while severed electric cables in the southwest halted train service and created traffic chaos. Interior Minister Bruno Retailleau reported nearly 200,000 demonstrators nationwide by evening, though the CGT union claimed closer to 250,000 participants. His ministry documented more than 450 arrests, hundreds in custody, more than a dozen injured officers, and upwards of 800 protest actions ranging from rallies to street fires. Retailleau declared the day “a defeat for those who wanted to block the country”, yet the government’s own statistics suggested otherwise.

The “Bloquons Tout” protests, while not matching the scale of France’s 2018 yellow vest movement, highlighted the recurring pattern of unrest during Macron’s presidency: Huge police deployments, violent outbursts, and persistent confrontations between government and citizenry. Since his 2022 re-election, Macron has faced intense public anger over controversial pension reforms, and nationwide riots following the 2023 police killing of a teenager in Paris’s suburbs. The demonstrations and intermittent clashes with riot police across Paris and beyond intensified the sense of crisis enveloping France after the government’s collapse on Monday, when former Prime Minister Francois Bayrou lost a parliamentary confidence vote.

The protests immediately confronted Bayrou’s successor, Lecornu, who took office on Wednesday. More than 80,000 police have been deployed as demonstrators rally against Macron’s government and austerity policies. The call to “block everything” came after former Prime Minister Francois Bayrou lost a confidence vote on Monday. Macron responded by appointing Defence Minister Sebastien Lecornu, a close ally, as his replacement. Lecornu is the fifth prime minister to be appointed in less than two years, and the fourth in just 12 months. Calls for Macron to resign spread nationwide
 
Sasa taona kama kweli na wenzetu huwa wanasikiliza raia wao.

Wananchi wanataka ajiuzulu chanzo ni kupunguzwa kwa bajeti n.k ila kifupi ni ugumu wa maisha.

Je Raisi atajiuzulu,maana kama ingetokea Africa kwa raisi wasiemtaka wangekuwa wameshatoa taarifa ya kumshauri asikilize wananchi.
 
Nadhani kwasasa ulimwengu unashuhudia mabadiliko ya kimamlaka katika kila jamii.

Mifumo ya kizamani ambayo haikidhi mahitaji ya kisasa na kulazimisha kuzuia mabadiliko inatolewa kwa nguvu.

Africa naona tupo slow sana kama vile tulivyochelewa kupata uhuru. Ila najua muda umefika.

Serikali nyingi zimeshindwa kudeliver mahitaji sahihi ya uhuru na Demokrasia kwenye jamii zake. Wale waliokuwa ni watoto au hawakuzaliwa kipindi cha uhuru saa hii wamekuwa ni watu wazima na wazee pia.

Wanashuhudia uzembe wa wazi wazi ambao unazorotesha ustawi wa jamii kwa makusudi kwasababu kuna famila za wendawazimu wachache wameishi kwa mazoea ya kupenda vya bure na wanataka sasa kuhalalisha na kulazimisha hali ibakie hivyo milele.

Nepal wameonyesha mfano mzuri sana kwa kuwatoa watu wa aina hii kwa viboko kama vile mkaidi yoyote yule ambaye anapoambiwa kwa heshima anaona anaogopwa then anatakiwa kuwajibishwa kivitendo tena kwa lazima.

Unapoishi jamii ya watu wastaarabu na waungwana unatakiwa kujiweka mkao huo huo na si kujiona wewe ni mwamba huu yao na unawamudu.

Muda ndio umefika tayari na hawa wendawazimu au wanaharamu wapenda dhuruma wanatakiwa kukutana na mkono wa kiboko cha wanajamii wanaojua kuadabisha na kufunza nidhamu na utu kwa nguvu.

Africa ni moja na tunafanana. Nina uhakika ni swala la muda mfupi sana jamii ya kila mwafrika katika kila kona itasimama na kuanza kuwaadhibu hawa wendawazimu ambao wamechagua kukanyaga katiba na kupuuza heshima ya uongozi katika jamii na kutumia mamlaka kujineemesha wao na familia zao.

Viboko vitembee kweli kweli. Tena viboko haswa. Video za Nepal zinaonyesha namna wanainchi wanatakiwa kuwashughulikia waharibifu wa taifa na wachezea katiba.

Kila siku tunapiga wezi wa kuku,simu, pochi,wezi wa viatu na nguo, tena tunawauwa ikibidi na kuchoma moto,lakini wezi wa mabilioni tunapaki magari yetu pembeni tukiwasubiri nusu saa zima wapite kwenda kupanga mipango ya kutufilisi rasilimali. Kwanini hatuwaadhibu kama wezi wengine?

Muda unakaribia jamii itaadhibu hawa wakaidi ambao hawakufunzwa vibaya na wazazi wao.

Asiyefunzwa na mama yake hufunzwa na walimwengu.
 
Ninachoona, Tarehe 29 Oct inawezekana wananchi wakaandamana ama wasiandamane, lakini ikitokea hawatoandamana , kutakua na wapiga kura wachache haijawahi kutokea kwenye vituo katika historia ya hii nchi....
 
Zaidi ya watu 200,000 wameandamana na mamia wakamatwa nchini Ufaransa Septemba 11, 2025 kufuatia maandamano makubwa ya kitaifa yaliyoanza Septemba 10, 2025 wananchi wakipinga mipango ya kupunguza bajeti na hali tete ya kisiasa nchini humo.​
Vuguvugu hilo lililopewa jina “Fungeni Kila Kitu” liligeuka kuwa mapambano makali, mitaa ikijaa moshi, vizuizi vya moto na gesi ya machozi. Hali hii imekuwa mtihani mzito kwa Rais Emmanuel Macron baada ya kumteua Waziri Mkuu mpya, Sebastien Lecornu.

Licha ya serikali kupeleka polisi 80,000 kudhibiti hali, vurugu zilisambaa kote nchini. Huko Rennes, basi liliunguzwa moto, huku nyaya za umeme zilizokatwa kusini magharibi zikisitisha huduma za treni na kusababisha msongamano mkubwa wa magari.

Waziri wa Ndani, Bruno Retailleau, alisema karibu waandamanaji 200,000 walishiriki, ingawa chama cha wafanyakazi cha CGT kilikadiria idadi hiyo kuwa zaidi ya 250,000. Kufikia jioni ya Septemba 10 polisi walikuwa wamewakamata zaidi ya watu 450, mamia wakiwa bado rumande, zaidi ya maafisa 12 walijeruhiwa, na zaidi ya matukio 800 ya maandamano yaliripotiwa kuanzia maandamano ya amani hadi moto mitaani. Retailleau alidai kuwa siku hiyo ilikuwa “ushindi dhidi ya waliotaka kufunga taifa,” lakini takwimu za serikali zilionesha hali tofauti.
​
Maandamano haya yamefufua kumbukumbu za vuguvugu la Yellow Vest mwaka 2018, na yanaonesha hali inayojirudia katika urais wa Macron: polisi wengi mitaani, ghasia, na mvutano wa kudumu kati ya wananchi na serikali.
Tangu achaguliwe tena mwaka 2022, Macron amekabiliwa na hasira kubwa ya wananchi—kuanzia mageuzi ya pensheni yaliyoibua upinzani mkali, hadi ghasia za kitaifa baada ya polisi kumuua kijana katika vitongoji vya Paris mwaka 2023.​

Maandamano ya wiki hii yamechochewa na kuanguka kwa serikali Jumatatu, baada ya Waziri Mkuu wa zamani François Bayrou kushindwa kwenye kura ya imani bungeni. Macron alimjibu kwa kumteua mshirika wake wa karibu na Waziri wa Ulinzi, Sebastien Lecornu, kuwa Waziri Mkuu mpya. Hii inamfanya Lecornu kuwa Waziri Mkuu wa tano chini ya miaka miwili na wa nne ndani ya mwaka mmoja pekee.

Sasa, kwa sauti za “Macron ajiuzulu” zimesambaa kote nchini, huku maandamano haya yakionyesha udhaifu wa uongozi wa kisiasa na hasira ya wananchi dhidi ya serikali.

===============For English Audience============​

France’s streets ablaze as antigovernment protests disrupt daily life Hundreds arrested after more than 200,000 demonstrators force French government into high-stakes confrontation. A protester displays a French national flag next to burning rubbish bins. A protester of the 'Block Everything' movement displays a French national flag next to burning rubbish bins in Lille, northern France.

A nationwide wave of antigovernment protests swept across France, filling streets with smoke, burning barricades and tear gas as demonstrators rallied against budget cuts and political instability. The “Block Everything” campaign created a formidable test for President Emmanuel Macron and transformed Sebastien Lecornu’s first day as prime minister into an immediate crisis. While the movement did not achieve its goal of total national disruption on Wednesday, it successfully paralysed significant portions of daily life and ignited hundreds of flashpoints throughout the country.

Despite deploying 80,000 police officers who dismantled barricades and arrested hundreds, disturbances multiplied across France. Protesters torched a bus in Rennes, while severed electric cables in the southwest halted train service and created traffic chaos. Interior Minister Bruno Retailleau reported nearly 200,000 demonstrators nationwide by evening, though the CGT union claimed closer to 250,000 participants. His ministry documented more than 450 arrests, hundreds in custody, more than a dozen injured officers, and upwards of 800 protest actions ranging from rallies to street fires. Retailleau declared the day “a defeat for those who wanted to block the country”, yet the government’s own statistics suggested otherwise.

The “Bloquons Tout” protests, while not matching the scale of France’s 2018 yellow vest movement, highlighted the recurring pattern of unrest during Macron’s presidency: Huge police deployments, violent outbursts, and persistent confrontations between government and citizenry. Since his 2022 re-election, Macron has faced intense public anger over controversial pension reforms, and nationwide riots following the 2023 police killing of a teenager in Paris’s suburbs. The demonstrations and intermittent clashes with riot police across Paris and beyond intensified the sense of crisis enveloping France after the government’s collapse on Monday, when former Prime Minister Francois Bayrou lost a parliamentary confidence vote.

The protests immediately confronted Bayrou’s successor, Lecornu, who took office on Wednesday. More than 80,000 police have been deployed as demonstrators rally against Macron’s government and austerity policies. The call to “block everything” came after former Prime Minister Francois Bayrou lost a confidence vote on Monday. Macron responded by appointing Defence Minister Sebastien Lecornu, a close ally, as his replacement. Lecornu is the fifth prime minister to be appointed in less than two years, and the fourth in just 12 months. Calls for Macron to resign spread nationwide
Urusi effect
 
Back
Top Bottom