Habar wakuu,amani iwe juu yenu
Wananchi mkoa wa Mara kijiji cha Nyamuswa wakiongozwa na wazir mkuu mstaafu jaji Sinde Warioba wameeandamana na kuweka mkutano kwa lengo la kumpongeza rais Magufuli kwa kusimamia rasilimali za taifa ipasavyo..wananchi hao walienda mbali zaid kwa kubeba mabango yanayomtaka rais Maguful aongoze miaka 100!
My take:Hata Rwanda walianza hivi hivi chondechonde watz wenzangu tuwe makini kuna harufu ya ukagame inanukia.
======
Jaji Warioba aongoza wazee kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli mkoani Mara.
Waziri mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba ameongoza wazee wa kijiji cha Nyamuswa wilayani Bunda mkoani Mara kuunga mkono juhudu kubwa zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt.John Pombe Magufuli katika kulinda rasilimali za taifa huku akiwataka watanzania kuungana pamoja katika mapambano dhidi ya maslahi ya taifa.
Wakizungumza mbele ya mkuu wa wilaya ya Bunda Bi. Lyidia Bupilipili,wazee na wananchi hao wa kijiji cha Nyamuswa,wamempongeza Rais John Pombe Magufuli katika kutetea rasilimali za Umma hasa katika uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu na hivyo kuwandolea kero ya michango ambayo ilisababisha kushuka kwa elimu katika eneo hilo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bunda Bi.Lyidia Bupilipili, akizungumza baada ya kupokea tamko hilo la wazee na wananchi wa kijiji cha nyamuswa kwa niaba ya Rais, amesema ni jukumu la kila mtanzania kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Rais John Pombe Magufuli hasa katika kutetea wanyonge.
Chanzo: ITV