Wananchi masikini wapewe kipaumbele kuset agenda za uchaguzi 2020

Wananchi masikini wapewe kipaumbele kuset agenda za uchaguzi 2020

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Wasalamu!

Tumeingia kwenye awamu nyingine ya kusaka viongozi wetu wa awamu ya tano/sita katika ngazi ya Urais,Ubunge na Udiwani.

Naipongeza Serikali chini ya Rais Shupavu John Pombe Magufuli kwa kitufikisha hatua hii kwa amani,usalama na Siha njema.Hili halikuwezekana hivi hivi bali kwa ujasiri,akili ,maarifa na kujifunza kwake kusikokoma.

Nchi ilipitia changamoto mbalimbali nzito na za aina ya kipekee.Nchi ilipitia matishio ya kugawanywa,kuhujumiwa kiuchumi,chembechembe za usaliti wa wazi,ugaidi,majanga ya hali ya hewa,njaa na hatimaye COVID 19 Pandemic.

Tukitafakari wagombea wa mwaka 2015 hasa yule aliyetaka tuamini kuwa ndiye angefaa utaona ni namna gani tulimuhitaji Rais tuliyenaye.

Tukiwatazama wabunge na madiwani wanaomaliza muda wao tunaweza kujua nani walikuwa real kwa maslahi ya wananchi wanyonge na nani waliingia kwa upepo tu na hivyo baada ya kuingia hawakufanya lolote.

Tumeshuhudia kuibuka kwa wanaharakati vibaraka na wadhalilishaji wanaodakia matukio mbalimbali na kuyatolea maoni yasiyo na utatuzi endekevu...yaani ni basket mouths na makasuku wa mambo yasiyo na tija kwa wavuja jasho na hufanya hivi kwa manufaa ya matumbo yao tu.

Niingie kwenye kuminanane kwa kuishawishi jamii hasa hii ya tunaojiita Great thinkers kwa kuwaeleza kuwa tutumie uwezo wetu kuwafikiria wasio na uwezo au wenye uhitaji wa yale ambayo baadhi yetu tumeyapata.

Yaani tufikiri kwenye ngazi ya familia hasa za pembezoni zinavyoishi na hatimae tuwatengenezee fursa na juhudi zao zilipe kwa manufaa yao na vizazi vijavyo.mfikirie mjamzito anayeishi kilometa 200 mwituni kutoka makao makuu ya wilaya kuifuata hospitali ama mahitaji muhimu.

Tukiwaza kwa muktadha huu hatutababaishwa na wanahabari failures au wanaharakati wachumia tumbo au vibaraka wa makampuni makubwa kuzisemea shida halisi za mtanzania.

Aidha tuondokane na hulka za kuiga iga upuuzi wa walami ndio tukafanya kuwa muelekeo endelevu wa Taifa.

Kwa kifupi tuweke agenda nyeti ya maendeleo ya vitu,miundombinu na watu kama dira ya aina ya viongozi tunaotakiwa kuwa nao.

Nitamdharau sana mwanasiasa au msomi au mtu maarufu atakayetaka kutulazimisha tuimbe nyimbo za miaka ya vita kuu ya dunia au harakati za ukombozi.

Nitamdharau mwanasiasa atakayetaka tuige nchi zinazopigania haki ya ndoa za jinsia moja n.k wakati umeme haupo kwenye baadhi ya maeneo.

Nitamdharau kiongozi wa dini kujidharaulisha kwa kudakia mada za kisanii na kutaka kuwaaminisha waaumini wake juu ya usanii huo.

Uzoefu katika miaka mitano unadhihirisha kuwa Tanzania ina resources zote yaani watu,watu wenye weledi,miongozo mizuri,maji,umeme tuli,mafuta tuli,ardhi kubwa,mawe na madini muhimu n.k vyote hivi havijawa explored ili kuleta tija ...

Awamu ya Rais Magufuli imetufunza jambo kuu yaani UWAJIBIKAJI na Uchapaji kazi unalipa.Pia USIMAMIZI (UONGOZI) sahihi unalipa.hivyo sio muda wa kukosea.

Kupitia waraka huu niwaase wahusika wote kwenye kilinge cha siasa kujikita kwenye hoja nzito ya kuwasaidia wananchi na tuwapime wagombea kwa muktadha huo.

Tusiwasemee wananchi tuwaache wayaseme ya kwao ambayo ni muhimu.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
 
Sisi Chadema tayari tumejiapiza kutowadharau wala kuwatukana watu masikini wanaokumbwa na majanga mbalimbali kama vile tetemeko au mafuriko
mtawafanyia nini kilicho endelevu?Usinitajie msaada wa debe la mahindi na kuchangisha mchango kwa Namba binafsi za Mpesa
 
Miaka mingi mtaji wa CCM ni huu.

Yani miaka 50 naaa leo ndio uwashauri hivyo, nadhani jibu jepesi ni kuwatoa ccm madarakani.
IMG_20200816_193531.jpg
 
tuambie miaka mitano hii zaidi ya kuwakejeli masikini kwenye majanga na kudhulumu korosho na mazao yao mengine mmewafanyia nini ?
Ipo thread maalumu ya kuonesha hayo ...hoja yangu ni namna gani agenda za wanasiasa zituelekeze katika kutatua changamoto zilizobaki
 
Ipo thread maalumu ya kuonesha hayo ...hoja yangu ni namna gani agenda za wanasiasa zituelekeze katika kutatua changamoto zilizobaki
Ukileta udikteta kwenye uzi wako patachimbika ! ni yapi mliyoyafanya yanayomnufaisha masikini , hata useme tujikite kwenye changamoto zilizobaki ?
 
Ukileta udikteta kwenye uzi wako patachimbika ! ni yapi mliyoyafanya yanayomnufaisha masikini , hata useme tujikite kwenye changamoto zilizobaki ?
Unataka nianzishe kampeni kwenye uzi huu??
Ni kweli huyajui yaliyofanyika?
 
Kwani bado masikini tupo? Mi nilidhan sisi walalahoi ni wale tuliokuwa wazee wa madili na vyeti feki nyie wakubwa wote mmehamia uchumi wa kati
 
Kwani bado masikini tupo? Mi nilidhan sisi walalahoi ni wale tuliokuwa wazee wa madili na vyeti feki nyie wakubwa wote mmehamia uchumi wa kati
Kufoji vyeti ni uhujumu uchumi
 
Swali ni je? Wanaokushabikia walijiandikisha na Wana vutambulisho vya kura ... Nakumbuka ufipa walipinga watu wasijiandikishe kwakua hakuna tume huru [emoji3][emoji3]
Hebu weka ile list ya viwanda 100@mkoa ili tupime unachoongea?
 
wazo zuri. Ila wapewe elimu kwanza maana wanaweza kuwa na matatizo lakini hawayatambui.
 
Back
Top Bottom