Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 611
- 567
Licha ya viongozi wa vyama na serikali kuhamasisha Wananchi kwenda kujiandikisha kwenye Daftari la Kupiga Kura, hali ni tofauti na matarajio yao.
Wananchi wamekuwa na mwitikio mdogo sana katika zoezi hilo na hii ni kutokana na Wananchi kuona hakuna umuhimu wa kupiga kura.
Nimepata bahati ya kupiga story na baadhi ya Wananchi ambao wamesema kuwa hawaoni umuhimu wa kwenda kujiandikisha na kuacha shughuli zao za kutafuta ridhiki.
Zoezi la uandikishaji katika daftari la mpiga kura limebakisha siku chache tu kukamilika lakini hali ilivyo Kwenye vituo ni kweupe peeee kabisa watu wako busy na shughuli zao za kila siku.
Nawaomba wananchi wenzangu tujitokeze kujiandikisha ili tupate nafasi ya kuchagua viongozi tunaowataka.