Hali ya sintofahamu imeibuka katika Jimbo la Mbarali, Mkoani Mbeya baada ya baadhi ya wananchi kutishia kususia Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025, wakipinga matokeo ya kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa madai ya kuwa mgombea aliyeibuka mshindi si chaguo lao, bali ni chaguo la chama, hali inayodaiwa kupuuzia matakwa ya wapiga kura halisi wa jimbo hilo
Kwa sauti ya pamoja wakazi hao wameuomba uongozi wa CCM Taifa kuingilia kati na kurejesha jina la mgombea ambaye kwa maoni yao ana uhalali wa kweli wa wananchi na ambaye wanaamini ataweza kuwaletea maendeleo endelevu, wakieleza kuwa matumaini yao yako mikononi mwa chama kusikiliza kilio chao ili kurejesha imani ya kisiasa katika eneo hilo
Aidha baadhi ya wajumbe wa kura za maoni, ambao ndio wapiga kura wa ndani ya chama wamesisitiza kuwa mchakato huo urudiwe ili kuhakikisha unakuwa huru, wa haki na unaoendeshwa kwa uwazi huku wakisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuondoa sintofahamu iliyojitokeza na kurudisha mshikamano wa wanachama kuelekea uchaguzi mkuu