PreGE2025 Wananchi Mtwara Mjini walalama Miaka mitano hawajawahi kumuona mbunge wao Jimboni, wanaishia kumuona kwenye Runinga

PreGE2025 Wananchi Mtwara Mjini walalama Miaka mitano hawajawahi kumuona mbunge wao Jimboni, wanaishia kumuona kwenye Runinga

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Wakuu vipi uko kwenye majimbo yetu?
Imekua tabia ya viongozi wengi kuonekana kipindi cha uchaguzi wakihitaji kura kutoka kwa wananchi huku wakitoa ahadi nyingi za maendeleo, ambapo baada ya uchaguzi ni kilio cha wananchi ndicho husikika na hii imewakuta wananchi wa Mtwara Mjini ikiwa ni miaka 5 sasa mbunge wao Hassan Mtenga kutokuonekana Jimboni
===

Wiki hii kwenye kipindi cha "KASWALI KANGU MPIGIE MBUNGE WAKO" tutakutembeza jimbo la Mtwara Mjini ambalo mbunge wake ni Hassan Mtenga na kuzungumza na baadhi ya wananchi pia kuwaunganisha na mbunge wao.

Moja ya mambo tuliyokutana nayo eneo la feri ni wananchi kudai kutokumuona mbunge wao toka aliposhinda uchaguzi 2020. Huku wengine wakisema wamemuona kwenye Runinga(TV).



Chanzo: JAMBO TV
 
Tayari alishashinda SASA mnataka kumuona WA nini?


Ni Kama vile umefunga goli alafu Unataka kukaa hapo hapo na kipa .mbunge ameenda kushangilia goli lake wananchi wasubiri shambuliz la October
 
Back
Top Bottom