LGE2024 Wananchi ni kama wamegoma kujitokeza kujiandikisha Olasiti, Arusha, kwani shida ni nini?

LGE2024 Wananchi ni kama wamegoma kujitokeza kujiandikisha Olasiti, Arusha, kwani shida ni nini?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257

Hivi ndivyo ilivyo katika Kata ya Olasiti pande za Chuga, jamaa ameshea video akionesha mwitikio ni mdogo sana, Wananchi wanajitokeza kwa uchache sana kujiandikisha.

Ndugu zangu kwani shida ni nini?
 
Huku kwetu imebidi wajumbe wa nyumba 10 na wenyeviti wa vitongoji wajaze boda Nafuta Kuwafuata watu majumbani.
Hao ndio baadae huwa wanalalama

Ni bora upige kura na uibiwe na dunia nzima ijue kuliko kutoa boko
 
Sio huko huku kwetu ndio balaa kwa serikali inayojielewa ilitosha kabisa kutoa ishara nini kinaendelea nchini lakini wao ndio kwanza eti wanabuni mbinu za uhamasishaji watu wajitokeze ,ifahamike kauli za wanasiasa wajinga ndio zimetufikisha hapa ,Waheshimiwa Wananchi wanaona wapigwe na jua mchana kutwa alafu kumbe wana mtu wao wa kumpitisha mfukoni nani atakubali? Wakapige wao na wake zao ma wakwe zao sasa
 
Nape na malkia wa nchi ya Guyana walisema nini juu ya matokeo ya kura?! kauli za hawa politicians zimesababisha wananchi wasijitokeze kujiandikisha
 
Back
Top Bottom