Wananchi Simiyu wawajengea walimu nyumba za matope

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
3,315
Reaction score
5,058

HABARI Wananchi wa Kitongoji cha Ihula kilichopo Kata ya Gibishi Halmashauri ya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu wameamua kujenga nyumba za tope ili kuwawezesha Walimu kuishi jirani na shule.

Wananchi hao wamesema walimu wakiwa karibu na mazingira ya shule wanao uhakikia wa kuwahi hususani vipindi vya asubuhi hivyo kuwawezesha watoto wao kuanza kufundishwa mapema.

"Tumeamua tujenge nyumba ili watoto wetu wapate huduma ya kufundishwa, hatuna nguvu ya kuwajengea nyumba ya block ndio maana tukaamua tujenge nyumba ya tope ili wasogee huku," amesema Loli Machama ambaye ni mwananchi
 
Duh! Huyu mother Nchi imemshinda kabisa.rasilimali zote tulizonazo ameshindwa kuzisimamia hadi watumishi kudhalilishwa kwa kujengewa nyumba za hovyo namna hiyo?bora ajiuzulu tu ili kulinda heshima.
 
Tope si tatizo ni design.
Hata Mimi nataka kujenga Goba ghorofa la tope.
Pana aina ya nyumba za tope zinaitwa Rammed earth House.
Juu naezeka kwa nyasi zilizopangiliwa vizuri.
Ukuta unajengwa kwa mgandamizo wa kuushindilia
 
Kwani tofali halitokani na tope? Mm sioni tatizo.

Lakini hebu tuulizane. Hivi ualimu nao ni kazi??
 
HABARI Wananchi wa Kitongoji cha Ihula kilichopo Kata ya Gibishi Halmashauri ya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu wameamua kujenga nyumba za tope ili kuwawezesha Walimu kuishi jirani na shule.

Wananchi hao wamesema walimu wakiwa karibu na mazingira ya shule wanao uhakikia wa kuwahi hususani vipindi vya asubuhi hivyo kuwawezesha watoto wao kuanza kufundishwa mapema.

"Tumeamua tujenge nyumba ili watoto wetu wapate huduma ya kufundishwa, hatuna nguvu ya kuwajengea nyumba ya block ndio maana tukaamua tujenge nyumba ya tope ili wasogee huku," amesema Loli Machama ambaye ni mwananchi

#EastAfricaTV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…