Wananchi Tabora wapongeza kliniki ya ardhi kidijiti, wapata hati miliki kwa muda mfupi

Wananchi Tabora wapongeza kliniki ya ardhi kidijiti, wapata hati miliki kwa muda mfupi

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165
74cbe686-d109-46db-8fd9-546f0e74dfb2.jpeg


TABORA

Wananchi mkoani Tabora wameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuwasogezea huduma za ardhi karibu kupitia Kliniki ya Ardhi Kidijiti, hatua iliyowawezesha kupata Hati Miliki kwa muda mfupi.

Wakizungumza baada ya kupokea Hati zao, wananchi hao akiwemo Bw. Mrisho Hamsini Magambo na Bw.Ramadhani Musa, wameishukuru Serikali kwa kuwajali wananchi na kuendelea kuboresha upatikanaji wa huduma za ardhi kwa kutumia mifumo ya kidijiti.

Aidha, wamewasihi wananchi wengine kutumia fursa hiyo kwa kufika katika Kliniki ya Ardhi Kidijiti ili kupata Hati Miliki pamoja na elimu kuhusu matumizi ya Mfumo wa e-Ardhi na masuala mbalimbali ya ardhi.

Kliniki ya Ardhi Kidijiti inaendelea mkoani Tabora hadi tarehe 3 Oktoba 2026 katika Viwanja vya TBC, ambapo wananchi wanaendelea kupata huduma na elimu mbalimbali za ardhi.
 
Back
Top Bottom