Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Watanzania wenzangu, kuna mengi ya kusikitisha yanayoendelea ndani ya nchi yetu na kubwa kuliko yote ni ukiukwaji mkubwa wa haki za msingi za raia wa taifa hili. Haki hizi ni zile zilizoorodheshwa ndani ya maazimio ya msingi tuliyokubaliana wananchi kama dira yetu na taratibu za maisha kijamii.
Tofauti na wanyama wa porini, binadamu huandaa namna ya kuendesha maisha yao kama mtu moja, familia na jamii katika taifa. Kufanikiwa katika hili kuna misingi tuliyoafiki kuijenga kama taifa na hivyo tumejiwekea sheria, kanuni na taratibu ambazo lazima zihifadhiwe, zilindwe na kutetewa na wote.
Ndio maana tunapomchagua kiongozi, tunahakikisha tunahodhi madaraka kama wanachi ya kumwajibisha kiutekelezaji kama ataenda kinyume na makubaliano yetu. Hivyo kitu cha kwanza kabisa anachotakiwa kufanya ni kuapa kwamba hatavuka mipaka ya uongozi kama iliyooainishwa ndani ya Katiba
Naomba nianze sasa kwa kunukuu Sehemu ya Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyosema kuhusu idara ya Mahakama...
107A.-(1) Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na Idara ya Mahakama ya Zanzibar, na kwa hiyo hakuna chombo cha Seriikali wala cha Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki.
(2) Katika kutoa uamuzi wa mashauri ya madai na jinai kwa kuzingatia sheria, Mahakama zitafuata kanuni zifuatazo, yaani:
(a) kutenda haki kwa wote bila ya kujali hali ya mtu kijamii Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (b) kutochelewesha haki bila sababu ya kimsingi;
(c) kutoa fidia ipasayo kwa watu wanaoathirika kutokana na makosa ya watu wengine, na kwa mujibu wa sheria mahususi iliyotungwa na Bunge;
(d) kukuza na kuendeleza usuluhishi baina ya wanaohusika katika migogoro; Uhuru wa Mahakama Sheria ya 2000 Na.3 ib.17
107B. Katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki, mahakama zote zitakuwa huru na zitalazimika kuzingatia tu masharti ya Katiba na yale ya sheria za nchi.
Tukiendelea hebu tujikumbushe alichoapa Rais John Pombe Magufuli baada ya kutangazwa na Tume ya Uchaguzi kuwa mshindi wa Urais November mwaka 2015...
"Mimi John Pombe Joseph Magufuli naapa kwamba nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nitalinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilivyowekwa kisheria.
Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie.
Mimi John Pombe Joseph Magufuli naapa nitatenda kazi zangu za Urais wa Jamhuri ya Tanzania kwa uaminifu kwa kutimiza wajibu wa kazi hizo kwa bidii na moyo mkunjufu na kwamba nitawatendea haki watu wote kwa mujibu wa sheria, mila na desturi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila woga, bila upendeleo, huba wala chuki.
Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie."
Kaimu Jaji Mkuu Prof Ibrahim Hamis Juma akiapa atakavyokuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano kwa kulinda uhuru wa Mahakama na kusimamia kikamilifu Mamlaka ya utoaji haki.
Jaji Mkuu ndiye Kiongozi wa Mahakama ya Rufani na pia Mkuu wa Idara ya Mahakama kama ilivyofafanuliwa katika ibara ya 116 ya Katiba.
Je ukimya wa Jaji Mkuu Katiba inaposiginwa, hati za mahakama kudharauliwa na haki za raia kuminywa kunatupa picha gani wananchi?
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali ambaye ndiye msaidizi maalum wa Jaji Mkuu katika utendaji wa kazi katika Mahakama Kuu na Mahakama nyinginezo zote za ngazi ya chini yake, na katika madaraka hayo Jaji Kiongozi atatekeleza kazi na shughuli atakazoagizwa au kuelekezwa mara kwa mara na Jaji Mkuu, na kwa madhumuni ya ibara hii, Jaji Kiongozi atajulikana pia kama Mkuu wa Mahakama Kuu.
Je ukimya wa Idara ya Mahakama, mawakili wanaponyanyaswa na vyombo vya dola na ofisi zao kushambuliwa tuutafsirije sisi raia?