Rais2020
JF-Expert Member
- Jul 14, 2016
- 3,248
- 5,537
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu, mahakama kama mahakama haifanyi kitu kama kutoa stop order badala au kama mbadala wa amri ya kuzuia kutu flani kisitendeke au kulazimisha kitu flani kitendekea. Kinachotokea ni mawakili wasio waaminifu au wasiojua kudanganya watena wao kwamba kuna kitu kinaitwa stop order kimetolewa na mahakama.Kama kweli Stop Order ya mahakama ni uhuni! Nini lengo LA mahakama kufanya uhuni huo?
Kama hujataka kufundishwa sitakufundisha. Nakupa homework yako hiyoNdo useme stop order ni nini?
Maneno meeeeeeeeengi
Dawa imeingia sawasawa?
Wewe naona ndo unayo mihemko. Unatiririka tu pasi kujua ukweli u wapi. Unahabari kuwa mahakama Hijaizuia serikali kubomoa?We unaangaliaga taarifa ya habari na hasa waathirika wa bomoa bomoa kimara au umekuja na mihemuko tu....[emoji15] [emoji15]
Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ndio unatka serikali ifanya kazi yake kwa kuangalia na kufuata visemavyo vyombo vya habari?
Sheria ipi imepuuzwa mkuuSheria za ndani zote zinapuuzwa.
Sheria za kimataifa ndio wanaziogopa.
Basi tuna safari ndefu sana na hali hii mateso hayatoisha kwa watawaliwa.@UncleBenMkuu nimeipenda Bandiko lako,Je huku ni watanzania wangapi wanaingia na kusoma??
Inabidi Katiba,Sheria na Haki za RAIA ziwekewe Makala kwenye Magazeti kama Vile Tanzania Daima,Mwananchi,Mtanzania nk nk.Najiuliza Waandishi wametutendea haki RAIA ??Au wako kwa ajili ya kusubiri appointment??
Hawa Mahakimu kwa sasa ni makada ni Mahakama ni Tawi la CCM, jiulize kesi ya CUF ni ya kuchukua miaka miwili bila kuhukumiwa??Nini nipo nyuma ya Mahakama na CUF??
Hata Mahakama wamechagua upande tayari hawako neutral.Kaimu Jaji na Jaji Kiongozi wamehsaamua kuchukua upande wa wanaowalipa marupurupu.
Najiuliza ni wanachama wa CCM tu ndiyo wanaolipa kodi??Kama siyo kwanini Bunge na Mahakama zimeamua kuchagua Upande wa Watawala?? Hivi tuna sababu ya watanzania kuwachagua wabunge au madiwani wa CCM kama hawawezi kusimamia Sheria na Haki.za RAIA??
Nimejiuliza hivi Kimara hadi Mbezi ni RAIA toka Taifa lipi?? Au kuna nchi inaitwa Chadema??Kama Rais anaweza kutoa Ujumbe ukapitia kwa.RC wa Mkoa husika na kusema.kwa.sauti Rais kanituma.hawezi Kuna wapiga kura wake wakiyeseka hivyo pande ile waliyompigia kura Nyingi hawatabomolewa nyumba zao.Wakimara wanapata Mateso sababu walichagua chama kile ambacho ni Taifa lingine haki itatendeka ndiyo sababu Kaimu Jaji kanyamaza.maana Kimara na Mbezi siyo RAIA wa Tanzania wala wapiga kura wa Rais
.
Kama kitu hukifahamu bora ukakaa kimya tu.
Stop order ni tofauti na amri ya zuio (Injunction). Tafuta mwanasheria akueleweshe, maana hapa unapinga tu badala ya kuomba ueleweshwe.
Basi tuna safari ndefu sana na hali hii mateso hayatoisha kwa watawaliwa.@UncleBen
mawakili gani wananyanyaswa na vyombo vya dola?Je ukimya wa Idara ya Mahakama, mawakili wanaponyanyaswa na vyombo vya dola na ofisi zao kushambuliwa tuutafsirije sisi raia?
Mmmh!Wananchi wapi hao waamke? Unajichosha tu na bandiko lako
Ni nyingi ndugu yanguSheria ipi imepuuzwa mkuu
Ni nyingi ndugu yangu
1.Stop order za mahakama kuhusu bomoa bomoa
2.Uhuru wa vyama vya siasa kufanya kazi zao.
3.Uhuru wa kupata na kutoa habari.
4.Suala la msajili kuviingilia vyama na kuvivuruga
Mkuu nasikitika umeandika pumba tupu.
- Bomoa bomoa inafanywa kwa mujibu wa sheria na hakuna mahakama imetoa zuio la kusitisha bomoabomoa. Hizi unazoziita stop order ni kiumbe gani katika sheria?
- vyama vya siasa vipo kwa mujibu wa sheria na vinatakiwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria katika harakati zao za kisiasa.
- Uhuru wa kutoa na kupata habari ni haki ya kikatiba kwa kila raia huru. Hata hivyo katiba inatoa analizo kwamba uhuru huu uwe kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.
- Msajili haingillii vyama, isipokuwa anafanya ukaguzi na urekebishaji kutokana na mamlaka aliyopewa na sheria ya vyama vya siasa.
.Mkuu nasikitika umeandika pumba tupu.
1.Kimara kulikuwa na stop order mkabomoa kwa mabavu
2.Vyama vyote vimepigwa marufuku kufanya mikutano yote mpaka 2020 kinyume na katiba.
3.Uhuru wa kutoa na kupata habari umekiukwa na sheria yenu ya kidhalimu ya makosa ya mtandao, kuficha taarifa za bunge bunge na kamata kamata zisozo na kichwa wala miguu.
4.Hujuma anazofanya Msajili na Lipumba dhidi ya CUF zinachefua.
Uje Kenya ujifunze demokrasia na utawala bora.
Aliyevimbewa hamjui mwenye njaa. Ipo siku utakuwa upande wa wanaonyanyaswa ndio utajua maumivu ya kunyanyaswa.
Tatizo unaandika bila mifano hai (sheria husika).
Halafu umesema uko kenya, kama ni hivyo basi ni ngumu sana kufahamu ya tanzania kwa sababu hata sheria za tanzania huzijui, na unaamini unayoyasikia kwenye mitandao ya kijamii tu. Malizeni kwanza ya kwenu huko.
- Nilisema na ninarudia tena kusema..: serikali haijazuiwa na mahakama kubomoa. Hiyo mnayoiita stop order ni uhuni tu na kamwa haiwezi kutumika kuzuia shughuli za serikali (au hata zangu mimi mtu bibafsi). unaweza kuniambia Stop order inatolewa au kuombwa kwa msingi wa sheria gani? Tafadhali tafuta mwanasheria unaemfahamu muulizie kuhusu hili. Sometimes naona itolewe elimu kwa umma kuhusu huu mkanganyiko -wanachi wanaangania kwa kutojua ukweli.
- Ni uongo ulio wazi kuwa vyama vyote vimepigwa marufuku kufanya mikutano ya kisiasa. Sijui umeambiwa na watu au unauhakika na hili? Kila siku vyama vya siasa vinaendesha mikutano yao ya kisiasa, kilichopo ni kuwa kuna mipaka ya kuendesha hizo siasa iliyowekwa.
- Kama nilivyosema awali, uhuru wa kutoa na kupokea upo kikatiba, sheria kama uliyoitaja ( ya mitandao) haiondoi uhuru huo uliowekwa kikatiba, isipokuwa inatoa muongozo wa kupokea na kutoa habari. Taarifa za bunge hazijafichwa, labda wewe ndugu yetu hujui namna ya kuzipata. Kamata kamata lazima ziendelee kwa sababu watu wanavunja sheria. Ingekuwa vizuri pia ungezitaja kamatakamata hizo hapa, pengine unangea kishabiki zaidi.
- Msajili kafanya hujuma gani CUF? kila kitu kinaenda kwa mujibu wa sheria, vinginevyo useme sheria (na kifungu) iliyovunjwa.
Mimi binafsi nimenyanyaswa sana, lakini nimegundua nimenyanyaswa kwa sababu ya makosa yangu na uzembe wangu mwenyewe. Sheria siku zote hainyanyasi mtu.A
Aliyevimbewa hamjui mwenye njaa. Ipo siku utakuwa upande wa wanaonyanyaswa ndio utajua maumivu ya kunyanyaswa