Wananchi tuanze rasmi kususia bidhaa na huduma za wasiolipa Kodi.

Wananchi tuanze rasmi kususia bidhaa na huduma za wasiolipa Kodi.

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Ndugu zangu wananchi wabunge hawalipi Kodi kwenye mishahara yao na ni mikubwa kwelikweli Sasa swali linakuja kwanini upande Basi lake? Kwanini ulale kwenye hoteli yake? Kwanini ununue chochote kwenye duka lake au hardware yake?

Tena Bora lingekuwa lile bunge lililochaguliwa na wananchi la kina sugu mbowe mnyika heche sio bunge hili lililotupandishia malipo ya MAKATO ya MIAMALA wakati wao hawalipi Kodi.

Operations hizi zianze mapema.

#KATAAWAKWEPAKODI#
 
Wakishiba hela zisizokatwa Kodi ndio wanakuja
Kututeka
Kutupiga risasi
Kupitisha Sheria kandamizi nk

Tuachane nao
 
Umekosea kidogo tafadhali rekebisha wazo lako,
Mimi sitasusia bidhaa za wakwepa kodi ambao ni raia wakawaida,bali nitasusia bidhaa za wanasiasa kwa ujumla wao,nitasusiaje bidhaa za raia wakawaida ambaye analipishwa kodi kandamizi za miamala?Wacha raia wakwepe ili walau wafidie pesa wanazolipishwa kwenye tozo za miamala ya simu.

Kwa yanayoendelea tz inatakiwa kutumia akili sana,yani mwanasiasa anashawishi raia alipe kodi halafu yeye amejitungia sheria asikatwe kodi kwenye mshahara wake!

Plz UKIENDA DUKANI USIDAI RISITI,UKIUZA USITOE RISITI.

Tufanye hivi mpaka wabunge wabadili sheria inayowapendelea wao kutokatwa kodi kwenye mishahara yao.
 
Tanzania hakuna mwanasiasa wa upinzani mwenye mvuto.

Kidogo Tundu Lisu ana kitu fulani. Ndio maana alipigwa risasi.
Yule anaweza akabadili upepo wa nchi kwa dakika.
Wengine ni wajanja janja tu hakuna kitu.

Zipo mbinu nyingi sana za kisiasa za kukabiliana na watawala dhalimu.


Kuhusu kususia bidhaa zao ni vyema Ukazitaja ili watu wazijue. Kama ni hotel basi ziwele wazi ili watalii wazijue pia.

Hata hivyo matajiri wote nyuma yao kuna wanasiasa wa chama tawala.




Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Kila mtu katika eneo lake ataje huduma na biashara zao tuanze kampeni sasa
 
Kila mtu katika eneo lake ataje huduma na biashara zao tuanze kampeni sasa
Hii imekaa vizuri,kila jimbo watajwe hata wale wafanyabiashara wapambe ambao huwa wanavifadhili vyama
 
Back
Top Bottom