Umekosea kidogo tafadhali rekebisha wazo lako,
Mimi sitasusia bidhaa za wakwepa kodi ambao ni raia wakawaida,bali nitasusia bidhaa za wanasiasa kwa ujumla wao,nitasusiaje bidhaa za raia wakawaida ambaye analipishwa kodi kandamizi za miamala?Wacha raia wakwepe ili walau wafidie pesa wanazolipishwa kwenye tozo za miamala ya simu.
Kwa yanayoendelea tz inatakiwa kutumia akili sana,yani mwanasiasa anashawishi raia alipe kodi halafu yeye amejitungia sheria asikatwe kodi kwenye mshahara wake!
Plz UKIENDA DUKANI USIDAI RISITI,UKIUZA USITOE RISITI.
Tufanye hivi mpaka wabunge wabadili sheria inayowapendelea wao kutokatwa kodi kwenye mishahara yao.