Kuelekea uchaguzi mkuu october 2025 no reform no election epewe airtime katika kipindi hiki , ili watawala wafanye marekebisho ya sheria zinazoitwa za uchaguzi zinazonufaisha chama tawala,
Huku kwa wananchi yule mama wana CCM wenyewe hawataki kumsikia habari zake na yule mzee wa totoz na bapa ambaye hanyoi nywele, sasa ili vyama vya upinzani viweze kushika dola huu ndiyo wakati wa kupaza sauti agenda ya no reform no election kila kona ya nchi, vyama vya upinzani vifahamu kwamba wapo wengi wanaowaunga mkono ndani ya CCM.
Ndani ya CCM wanachama wanasema kuwa aliyopo juu anaweza kufanya chochote bila kufuata katiba ya chama mfano mzuri mmeona mzee malisa alivyofurushwa baada ya kutoa maoni yake jinsi mkutano mkuu ulivyokiuka katiba ya kuwapata wagombea wa uraisi mwaka huu.
Wananchi tuamke viongozi wa ccm wameshakuwa genge la wahalifu tangu tumepata uhuru wamekuwa kazi yao ni kuuza rasilimali za nchi. haitoshi kwa sasa ukiwapinga uwe mpinzani uwe ndani ya ccm kwako unalala macho mda wote unaweza kuvamiwa au kuchomewa nyumba.
Sasa ndugu zangu ni wakati wa kuikataa ccm maana chama hicho kinaongozwa na genge la wahalifu wa mali za umma ambao hawachukuliwi hatua yoyote , chama hicho kimekuwa neema na ulaji wa familia zao ndugu na jamaa bali si kwa watanzania wote.