Wananchi tunamsaidiaje Mpina?

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Bila ya kujali itikadi, sote wananchi tuungane katika uzi huu kulaani kwa kauli moja uonevu wa spika dhidi ya Mpina.

Shime watanzania kila mtu aandike katika uzi huu maneno yafuatayo:
"NASIMAMA NA MPINA",

Hii itasaidia kumtia moyo Mpina na kumshinikiza spika Tulia kuachana na njama zake za kumnyamazisha.

NB: Huu siyo uzi wa kupiga stori, andika hayo maneno matatu tu. Comment ya kwanza nimeonesha mfano.

Mpina Spika Bashe.jpg

PIA SOMA
- Spika Tulia amburuza Luhanga Mpina Kamati ya maadili

- Luhanga Mpina apewa siku 10 na Spika kuleta ushahidi wa Bashe kulidanganya Bunge

- Luhaga Mpina: Usambazaji wa sukari haukuwa ukifanywa na mfanyabiashara mmoja wa Mwanza pekee, Waziri Bashe alidanganya

- Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia
 
Bila ya kujali itikadi, sote wananchi tuungane ktk uzi huu kulaani kwa kauli moja uonevu wa spika dhidi ya Mpina.

Shime watanzania kila mtu aandike ktk uzi huu maneno yafuatayo:-
"NASIMAMA NA MPINA",

Hii itasaidia kumtia moyo Mpina na kumshinikiza spika Tulia kuachana na njama zake za kumnyamazisha.

N.B. Huu siyo uzi wa kupiga stori, andika hayo maneno matatu tu. Comment ya kwanza nimeonesha mfano.
Taarifa ya Mpina ni ya hakika na inapaswa kuungwa mkono, lakini Mimi huwa siungi mkono watu walioshiriki dhuluma kipindi cha dhalimu magu. Hivyo aungwe mkono na wananchi, lakini mimi na watu wa dhuluma hapana.
 
Jeuri ya CCM kuiba bila aibu ni kwa sababu wana uhakika wananchi hawana cha kuwafanya. Kule Kenya wameungana wanaita Vamia Bunge.

Nukuu ya Kenyata ipo sawa...Nyerere anaongoza maiti
Mengine yote upo sawa mkuu 'OKW', isipokuwa hilo la Kenyatta.

"Maiti" wasingeweza kuwasambaratisha Wareno, Makaburu na wengine.

Huyo huyo Kenyatta, Idd wa Uganda alipodai mpaka kupitia Kisumu, kakimbilia kuomba msaada Uingereza; waTanzania aliowaita maiti wakamsaidia kufanya hiyo kazi!

Siyo busara kuwabeza waTanzania wakati wowote. Watafanya kazi yao wakati maalum. Vuta subira.
 
Taarifa ya Mpina ni ya hakika na inapaswa kuungwa mkono, lakini Mimi huwa siungi mkono watu walioshiriki dhuluma kipindi cha dhalimu magu. Hivyo aungwe mkono na wananchi, lakini mimi na watu wa dhuluma hapana.
Mkuu ni kweli. Lkn watu hujifunza kutokana na makosa na kisha hubadilika.

Hata shetani alikuwa malaika mkuu. Je, tuendelee kuheshimu asili yake (alipokuwa malaika) ama tumhukumu kwa kazi zake za sasa?
 
Back
Top Bottom