Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 652
- 1,058
Inasikitisha sana sana. Kuanzia Mkulu wa Nchi, Spika, Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu wa Sirikali, Mkuchika wa Utumishi, Waziri anayehusika na masuala ya kazi. Hawa wote wamejaa ukomoaji. Wanaendesha uongozi wa ki-imla. Wakati Mkulu akidai ananyoosha nchi wananchi wananyanyasika hasa.
Hawa wengine kwenye maeneo yao watu wao wananyanyasika bila kikomo (Mkuchika watumishi chepechepe, Mwanasheria Mkuu wa Serikali unawaliza wanasheria wenzako, DPP umekuwa mporaji wa kibabe, Spika unanyanyasa wapinzani sana, Mhagama vipi haki za wafanyakazi na nyongeza za mishahara yao una cha kusema miaka mitano hii?). Sijawasahau Polisi na yule sijui Mkurugenzi wa Mashtaka ambao wote wana mlengo wa kuwanyanyasa na kuwaonea wenye haki.
Ukweli hata sisi tulio kijijini tunaona mnavyonyanyasa watu kwa mgongo wa kwamba mnaleta ukombozi wa kiuchumi. Muda ni Jaji mzuri kuliko Prof. Ibrahim Juma. Leo nyie kesho wengine!