JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Licha ya mradi huo unaoratibiwa na Shirika la Reli Tanzania (TRC), kujenga baadhi ya vivuko vya juu kwenye baadhi ya maeneo, lakini baada ya kubaini umbali uliopo kutoka daraja moja hadi jingine (njiapanda ya Segerea na Magereza) waliamua kuweka karabati la chini eneo la Banana ambalo linatumiwa na wananchi kwa sasa.
Hata hivyo eneo la karabati ni kero kubwa kwa kuwa ni fupi na lina uwembamba ambao unasababisha tuvuke kama tunaruka kichurachura au wengine wakiwa wameinama licha ya eneo hilo kuwa refu karibia Mita 20.
Wanawake hususani wakina Mama wajawazito, wamama wenye watoto na wazee wamekuwa wakipata tabu.
Vilevile eneo hilo wamekuwa wakikatiza Watoto wa Shule, ambapo baadhi ya Wazazi wamekuwa na hofu ya Watoto wao kukabwa kwenye eneo hilo kwa sababu ndani kuna giza na eneo ni finyu, hali ambayo inaweza kupelekea baadhi ya watu wasio na nia njema kutendea uharifu.
Tunaomba mamlaka za juu ikiwemo Wizara ya Uchukuzi walifuatilie kwa ukaribu eneo hilo, kwani tumelalamika mara nyingi lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.
Ufafanuzi wa TRC ~ Kadogosa: Changamoto ya Vivuko kwenye reli ya SGR ipo, vitajengwa vingine hivi karibuni