The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Jeshi la polisi [TANPOL] lenye jukumu la kikatiba na kisheria kulinda usalama wa raia na mali zao limekana kuhusika na ukamataji wa watu hovyo nje ya utaratibu wa kisheria kisha kuwapeleka kusikojulikana, kuwatesa na baadae kuwaua na kutupa miili yao porini au nyikani.
Kama ndiyo hivi, maana yake ni kwamba watu hawa ambao mara zote wanapomwendea mlengwa wanaotaka kumtesa au kumuua hujitambulisha kama polisi. TANPOL imekana kuwa sio wao. Kama ni hivi, maana yake hawa watu ni kikundi cha uhalifu na ujambazi tu..
Lakini inashangaza zaidi kuwa TANPOL pamoja na kuwa jukumu lao la msingi ni kupambana na uhalifu kama huu, lakini wameshindwa kukidhibiti kisha kukitia nguvuni kikundi hiki cha kigaidi. Kwa sababu wanapofanya uhalifu huu kwa jina la "POLISI" maana yake wanajii - impersonate na kutumia jina la mtu mwingine kufanya uhalifu au tendo lilote, ni kosa kisheria.
Cha ajabu na cha kushangaza kabisa, polisi hawaoni kuwa hiyo ni shida na wanapaswa kushughulika nayo badala yake wanajibu kirahisi tu "Jeshi la polisi halihusiki.
Haya majibu yanaingia akilini kweli ndugu zangu?
Ushahidi ni matukio yasiyoisha na wahusika wanaotenda uhalifu huu kutokamatwa hata mmoja na TANPOL pengine hawafanyi hata uchunguzi.
Shida hii ilianzia mwaka 2017 pale ambapo kikundi hiki kilijaribu kumuua mwanasiasa, mwanasheria na mwanaharakati maarufu sana Tundu Lissu saa 7 mchana kweupe katika eneo la makazi ya viongozi AREA D - Dodoma.
Polisi hawajawahi kuchunguza wala kuchukua hatua zozote kwa wahusika wa tukio hili la kinyama kabisa kuwahi kutokea Tanganyika tangu enzi za ukoloni huku ushahidi ukiwa wazi kabisa na vidole vikiwaelekea baadhi ya viongozi wa serikali.
Mimi naamini kabisa kuwa, kikundi hiki cha uhalifu na ujambazi ni project mahususi ya viongozi wakubwa wa siasa walioko ktk Chama Cha Mapinduzi - CCM na serikalini na ktk vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hii kwa ajili ya kupambana na wanaowaona tishio ktk mipango yao ya kupata na kuendelea kubaki ktk madaraka yao ya kisiasa.
Soma Pia: Kupotea Kwa wananchi kadhaa na serikali kuamua kukaa kimya, tafsiri yake ni kuwa wananchi tutaamini kuwa, serikali yetu inahusika!
SASA WANANCHI TUFANYE NINI?
Jeshi la polisi (TANPOL) katika eneo ni wazi hawataki kushughulikia au wameshindwa kuushughulikia uhalifu huu kwa sababu wakubwa wao wanahusika. Sasa wananchi tunapaswa kuwasaidia kufanya kazi yao ya kisheria na kikatiba.
Na kwa maoni yangu wananchi tuchukue jukumu la kujilinda wenyewe kwa kutumia akili na hekima aliyotupa Mungu.
Kwanini tukubali vijana wetu, watoto wetu, baba zetu, mama zetu wakamatwe, wateswe na wapotezwe na kisha kuuwawa na majambazi hawa "kwa jina la polisi" kizembe na kirahisi hivi?
TUWASAIDIE POLISI KUFANYA KAZI YAO NA HIZI NI BAADHI YA MBINU ZA KUZITUMIA ILI HAWA WASIOJULIKANA WAJULIKANE:
1. Ukiipokea vitisho kwa yeyote vya "tutakushughulikia", mosi wataarifu jamaa zako wa karibu na weka rekodi ya namba za simu na sauti ya kila anayekupigia simu za namna hiyo.
2. Usiwe mwepesi kuitikia wito wa kwenda popote bila uchukua tahadhari muhimu.
3. Kama wanakufuata nyumbani, kwa sababu utakuwa unazo taarifa za kufuatiliwa, basi weka kundi la watu tayari watakapokuja na kutaka kufanya lolote.
4. Kama wanaokuja watajitambulisha kuwa ni polisi na wakaonesha ID zao. Hakiki kituo cha polisi wanachotoka na confirm na mkuu wa kituo hicho kabla hawajafanya lolote. Ukipata uhakika wa haya, hao ni polisi unaweza kwenda nao kituoni.
5. Kama waliokuja kukukamata wakijidai ni polisi na ktk utambulisha uka suspect vitu vusivyo vya kawaida, na ukawatilia shaka piga kelele na tulio karibu na kwa sababu tumejipanga na tumejiandaa, haraka sana tutafika na kukabilana nao hata kama wana silaha nyingi kiasi gani.
6. Tujipange na kuunda vikundi kukabiliana na majambazi haya. Hawawezi kutushinda. Ni wakati wa kuya - arrest na kuwatambua hawa watu ni kina nani na wanatumwa na nani. IINAWEZEKANA, TUAMUE TU maana polisi wameelemewa na jukumu hili.
7. Tutumie njia mbalimbali za mawasiliano kupeana taarifa ikiwemo WhatsApp groups, simu nk