DOKEZO Wananchi wa Bunda tunakumbana na rushwa iliyokithiri katika Mahakama ya Mwanzo ya Mcharo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Wananchi wa Kata ya Mcharo, Wilaya ya Bunda, wanaomba mamlaka husika kuchunguza tuhuma za rushwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Mcharo.

Kwa mujibu wa madai yao, baadhi ya wananchi hukosa haki kutokana na kushindwa kutoa rushwa. Pia kuna tuhuma kwamba baadhi ya wanawake wanaofuatilia mashauri yao hudaiwa fedha au vitendo vingine visivyofaa ili wapate haki wanayoistahili.

Wananchi wanadai kuwa vitendo hivyo vinahusisha ushirikiano kati ya hakimu wa mahakama hiyo na mtu anayetambulika kama karani au mwanasheria wa kata, anayefahamika kwa jina la Emmanuel Kitereja Mwanaamina.

Kutokana na uzito wa tuhuma hizi, wananchi wanaomba taasisi husika, ikiwemo TAKUKURU na Mhimili wa Mahakama, kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli na kuchukua hatua stahiki endapo madai hayo yatathibitika.
 
Huyo hakimu anaitwa nani?!
 
Back
Top Bottom