Wananchi wa Dar es salaam tuipime CCM na viongozi wake kupitia mvua hizi zinazoendelea kunyesha

Wananchi wa Dar es salaam tuipime CCM na viongozi wake kupitia mvua hizi zinazoendelea kunyesha

Wakuu

CCM na viongozi wake wamekuwa wakijinadi kipindi cha uchaguzi kwamba jiji la Dar es salaam limejengwa kisawasawa na miundombinu yake hususani barabara iko vizuri jiji zima

Fly over za kutosha, bombadi, daraja la salenda halikadhalika Mwendokasi vyote hivi CCM inasema ni kwaajili ya manufaa ya wanadaslam!

Mvua hizi zimekuja wakati muafaka, kipindi cha kampeni ambapo Magufuli na CCM yake wanasema waliahidi na wametekeleza, Je Jijini Dar es salaam waliahidi mafuriko kwa wakazi wa keko, mikocheni, jangwani na kwingineko?

Je waliahidi na kutelekeza barabara hizi zilizofungwa kufuatia mvua ya siku moja tu?

Ni muda muafaka sasa kwa wakazi wa Dar es salaam kuamua kuendelea kuteseka na hadha hizi za miaka mingi ndani ya jiji au kuchagua upande mwingine ili ukawatatulie kero hii kubwa kwani CCM imeshindwa
Unaacha kuweka huduma za msingi kama mitaro ya maji machafu unajenga flyover?!!!
 
Mvua ya Jana ni jaribu tosha kwa ccm dar! Nyakati Fulani bungeni wabunge watokao dar waliwahi kuomba jiji la dar litengewe fedha za ujenzi wa miundombinu ikiwepo mitaro mikubwa ya kupotosha maji ya mvua kuelekea baharini lakini hoja Ile ilitupwa mbali!
Jana peke yake madaraja ya kivule Tena mapya kabisa yameondoka na maji na huko kawe alikokuwa Leo watu walilala na maji ya mvua majumbani mwao!
Na bado ana guys za kuomba kura zao! Hii Kama siyo kebehi ni Nini?
Mvua hizi zilizoanza Jana zikiendelea ccm watatafutana kwenye ushindi!
 
Wakuu

CCM na viongozi wake wamekuwa wakijinadi kipindi cha uchaguzi kwamba jiji la Dar es salaam limejengwa kisawasawa na miundombinu yake hususani barabara iko vizuri jiji zima
Miundo-mbinu ya uhakika jijini Tokyo kupambana na mafuriko yaletwayo na maji ya mvua kubwa . Miundombinu hiyo chini ya ardhi imefananishwa na "Hekalu Kubwa" kutokana na ilivyosanifiwa huku nguzo kubwa zikileta mfananisho wa hekalu. Jiji la Tokyo lina wakaazi milioni 30 yaani mara tano idadi iliyopo ya wakaazi wa jiji la Dar es Salaam lenye watu milioni sita.

: tazama ma-injinia walivyojenga mfumo wa miundombinu kuzuia mafuriko jijini Tokyo katika video hii chini:

28 October 2014
Tokyo, Japan

Tokyo Flood Prevention | Insane underground tunnel system in Japan!


Fifty metres under Tokyo lies a subterranean world — 6.4 kilometres of tunnels, water tanks and massive pillars constructed to withstand 200 tonnes of water per second. This engineering marvel built to protect the ever-present threat of Tokyo flooding.
Source: ABC Science
 
CCM wanasema wamejenga flyover nyie mnalalamika mafuriko, mta watoa roho hawa watu mwaka huu.

Mvua zinawaaibisha na maendeleo yao ya vitu.
 
Sisi wakazi wa dar es salaam tunatambua kuwa mafuriko sometimes ni act of God. Ndio Maana sometimes ni hata London pia,Husumbuliwa na Mafuriko mara kadhaa.

Isitoshe MiundoMbinu ya barabara hii iliyojengwa imesaidia sana baadhi ya maeneo na nina Experince baadhi ya Maeneo ya M/Nyamala ambapo mwanzo mvua ikinyesha tu basi Nyumba inageuka boti isiyoelea. But now hili tatizo lime be solved baada ya kupata mitaro mikubwa along to these roads.
 
Kutoka Tazara kuelekea ubungo kulikuwa hakupitiki. Kuna mafaraja hapo kati yalikuwa yamefurika hata hujui daraja au barabara iko wapi
We tatizo lako unapita chocho ungepita UBUNGO au Tazarra
 
Hizi mvua zimeletwa na wapinzani ili kuvuruga ziara ya JPM DSM, na pia kuvuruga hoja ya ujenzi wa flai over na miundombinu DSM, nimesikia wapinzani wameleta kikosi ya waganga wa kuita mvua ili mvua inyeshe mfululizo mpaka tarehe 26/10, ili wana DSM waichukie serikali baada ya kupigwa na shida ya foleni.

Nasikia eti kila sehemu mzee wetu akienda kuhutubia, hawa waganga wanaanza kazi siku moja kabla, na wakiona watu hawasikii, wataanza kuleta ngurumo kubwa kama za kuzimu pamoja na radi kali zinazowaka mwanga kutoka kusi mpaka kaskazi

Sie wana ccm na sisi tutafute waganga wa kuzuia mvua, Mshana Jr tafadhali, hebu ingia uwanjani,wazee wenzio hatuwezi kuadhirika na wewe upo, Fanya mafekeche mvua zikiletwa na hawa jamaa basi unazielekezea baharini
Daaaaaah.
 
Takwimu zinaonyesha Dar es salaam ndo Mkoa hapa Tanzania unaoongoza kwa kukaliwa na watu wengi wenye upeo mdogo hapa Tanzania.
Ndo Mkoa unaokuta jitu linatiririsha maji machafu ya chooni barabarani, linatupa taka ovyo na bado hilo jitu litajitokeza hadharani kulaumu Serikali kuwa Jiji linanuka na CCM iondoke madarakani.
Hivi kwani Dar ina jumla ya wapiga kura halali wangapi kwa mujibu wa Tume?
 
Kero niliyoipata jana kutokea mjini sina hamu na hawa jamaa; how comes unatoka Kariakoo saa 10 jioni unafika viunga vya jiji saa 6 usiku? Wahusika oneni aibu basi; ni kero ya kila mara lakini hamjifunzi.
Drainage system ya hili jiji ni mbovu haswa. Ukweli mgumu ni kwamba sehemu kubwa ya jiji hususani maeneo ya mjini kati imejengwa kwenye njia za maji. Huwezi zuia mafuriko
 
Back
Top Bottom