KERO Wananchi wa Eneo la Iduda, Mbeya tunateseka na tatizo la kukatika kwa Umeme

KERO Wananchi wa Eneo la Iduda, Mbeya tunateseka na tatizo la kukatika kwa Umeme

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wananchi wa eneo la Iduda, Jiji la Mbeya, hususan maeneo yanayozunguka Shule za Msingi na Sekondari Iduda, tunakabiliwa na tatizo kubwa la kukatika kwa umeme mara kwa mara.

Kwa wastani, tunapata umeme kwa takribani siku nne pekee kati ya siku saba za wiki. Tumekuwa tukipiga simu mara kwa mara kupitia huduma kwa wateja namba 180, lakini hadi sasa tatizo hilo halijapatiwa suluhisho la kudumu.

Watoa huduma kutoka Uyole wamekuwa wakitueleza kuwa kuna hitilafu kwenye laini yetu, lakini tatizo hilo limeendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja bila kutatuliwa. Tunaelezwa pia kuwa laini hiyo inahudumia upande wa Makete na ina changamoto kubwa.

Tunaomba Wizara na mamlaka husika ziliangalie suala hili kwa haraka na kuchukua hatua za kutatua tatizo la laini hiyo, ili wananchi wa Iduda wapate huduma ya umeme ya uhakika na ya kudumu.
 
Habari, ndugu mteja.

Kwanza, tunaomba radhi kwa kuchelewa kukupatia mrejesho kuhusu changamoto uliyoeleza.

Tafadhali fahamu kuwa TANESCO inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme katika mkoa wa Mbeya. Tarehe 11 Septemba 2026, kwa mfano, mkataba wa ujenzi wa miundombinu muhimu ya umeme ulisainiwa, ikiwa ni sehemu ya hatua zinazolenga kuimarisha upatikanaji na ubora wa huduma ya umeme.

Mradi huo unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolti 220 (220kV) kutoka Iganjo, Mbeya hadi Saza, yenye urefu wa takribani kilomita 122, kwa thamani ya TSh bilioni 109. Aidha, unahusisha ujenzi wa kituo cha kupozea umeme chenye uwezo wa 100MVA, sawa na takribani MW 80.

Kukamilika kwa mradi huu kunatarajiwa kuongeza uwezo wa miundombinu ya umeme na kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto za upatikanaji na ubora wa umeme zinazowakabili wateja katika maeneo husika.

Hivyo, tunaomba muendelee kuwa na uvumilivu wakati hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huu zikiendelea.

Tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza, tukiamini huduma itaimarika baada ya mradi.

Asante. ^HN
 
Back
Top Bottom