KERO Wananchi wa Igoma, Mwanza, tunakabiliwa na changamoto ya usafiri wa daladala kwenda maeneo mbalimbali

KERO Wananchi wa Igoma, Mwanza, tunakabiliwa na changamoto ya usafiri wa daladala kwenda maeneo mbalimbali

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi wananchi wa Igoma, Mwanza, tunakabiliwa na changamoto ya usafiri wa daladala kwenda maeneo mbalimbali, ikiwemo katikati ya jiji, Buhongwa, Airport na Ilemela.

Kwa sasa, tunategemea daladala zinazotoka Kisesa au Kishili. Hata hivyo, zinapofika Igoma huwa tayari zimejaa, hali inayosababisha usumbufu na changamoto kubwa kwa wananchi wanaohitaji kusafiri kwenda maeneo hayo.

Kwa kuzingatia ongezeko la watu na shughuli mbalimbali katika eneo la Igoma, tunaomba mamlaka husika zifikirie kuongeza daladala zinazoanzia Igoma ili kukidhi mahitaji ya usafiri ya wananchi.

Hatua hiyo itasaidia kupunguza msongamano, kurahisisha usafiri na kuboresha huduma ya usafiri wa umma kwa wananchi wa Igoma.
 
Back
Top Bottom