Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Wananchi wa Kijiji cha Karema wilayani Tanganyika, mkoani Katavi, wameishukuru Serikali chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwajengea kizimba maalum pembezoni mwa Ziwa Tanganyika ili kukabiliana na changamoto ya mamba waliokuwa wakiwaua na kuwajeruhi wananchi kwa muda mrefu. Shukrani hizo zilitolewa Oktoba 17, 2025, wakati wa usimikaji wa kizimba hicho kilichojengwa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa lengo la kupunguza migongano kati ya binadamu na mamba.
“Wananchi wanapaswa kuepuka kutupa taka au mabaki ya chakula ziwani kwani huchochea mamba kusogea karibu na maeneo ya shughuli za binadamu. Pia wasifanye kazi majini nyakati za jioni,” amesisitiza Moshi. Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kijiji cha Karema, Juma Iddi ameishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia TAWIRI kwa kusaidia ujenzi wa kizimba hicho, akiahidi kuwa watahakikisha kinatumika ipasavyo. “Tulikuwa tunaishi kwa hofu kubwa, hasa wanawake na watoto waliokuwa wakifanya shughuli ziwani. Tunamshukuru sana Mhe. Rais Samia kwa kutuondolea adha hii ya muda mrefu,” amesema Iddi.