Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Siku chache baada ya RC Makonda kuelekeza TAKUKURU wamweke ndani Mtendaji Kata ya Bwawani na asipewe dhamana kwa tuhuma za kuchukua rushwa milioni moja; wananchi wa kati hiyo zaidi ya mia mbili wamekodi magari na kwenda ofisi za TAKUKURU kushinikiza mtendaji huyo aachiwe huru kwani mafisadi wakiongozwa na madiwani na viongozi wa CCM waliofisadi kata hiyo wameanza kutumia ulaghai kuwakandamiza wananchi.
Wananchi wamesema mtendaji huyo alipangiwa kufanya kazi kata hiyo mwaka 2019. Alipoanza kazi mashamba ya kijiji yalikuwa yanatumika na viongozi kulima na kujimilikisha kama ya kwao. Mtendaji aliwanyang'anya mashamba hayo viongozi akiwemo diwani na kuwapa wananchi jambo ambalo viongozi hao wa CCM walichukizwa nalo.
Wakati anapangwa kufanya kazi katika kata hiyo hakuna fedha iliyokuwa inakusanywa kama ushuru kutoka kwenye mali za kata; kwa sasa mashamba yanachangia zaidi ya milioni 30.
Amefanikisha kujenga kituo cha afya na shughuli za maendeleo zinaendelea. Aidha, wakati anaingia wanafunzi walikuwa wanapeleka mahindi na maharage kwa ajili ya chakula ila sasa hivi mtendaji huyo ametenga ekari 20 kwa ajili ya shule na kwa mwaka huu shule imevuna zaidi ya gunia 80 zinazotumika kulisha wanafunzi.
Kuhusu rushwa ya milioni moja inayodaiwa na Mkuu wa Mkoa, wananchi wamesema fedha hizo zilitolewa adharani na hazikuwahi kukabidhiwa kwa mtendaji badala yake zilielekezwa kununua vifaa vya ujenzi na kwamba Makonda alipaswa kuwahoji wananchi kuliko kutoka na taarifa ofisini kwake na kwenda kuwakamata watu wasio na hatia kwa maelekezo ya mafisadi wanaotumia mali za umma kuwaumiza viongozi wenye maono kama mtendaji.
Wananchi hao wameitaka TAKUKURU kufanya kazi kwa utaalamu badala ya kufanya kazi kisiasa. Wamehoji kama kweli kulikuwepo rushwa kwanini TAKUKURU haikuwahi kuchunguza badala yake inapokea maelekezo? Wamehoji kwanini TAKUKURU wameshindwa kufika kijijini kufanya mahojiano na wananchi badala yake wamejazana kumweka mahabusu mtendaji ambaye dhamana ni haki yake?
Mwisho, wananchi wanadai mambo aliyoyafanya mtendaji wa Bwawani yanastahili pongezi na siyo kuadhibiwa kama mkuu wa Mkoa anavyofanya. Kama mkuu wa mkoa ana vyombo alipaswa kubaini mapema kwamba viongozi wa CCM wa kata wanatumia ofisi yake kupambana na watendaji wa serikali wanaowatumikia wananchi kwa haki.