Nani huyo aliagiza Mahakama isimpe dhamana?Amefikishwa mahakamani lini?Hizi hearsay na vikao vya kahawa ni matatizo makubwa. Get your facts right.Acha kukurupuka na kusikiliza viredio mbao.Tena kwa kuiagiza mahakama isimpe dhamana! Upuuzi mtupu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nani huyo aliagiza Mahakama isimpe dhamana?Amefikishwa mahakamani lini?Hizi hearsay na vikao vya kahawa ni matatizo makubwa. Get your facts right.Acha kukurupuka na kusikiliza viredio mbao.Tena kwa kuiagiza mahakama isimpe dhamana! Upuuzi mtupu
Sure.Nchi inashangaza kiongozi atoke huko apelekwe Arusha , bora kuacha wan-Arush watafute kiongozi miongoni mwa jamii zao ndio tatizo mpaka mkurugenzi wa jiji ni mwizi.
Na kasema kila tuhuma ya jinai?Kusoma na kuelewa ni muhimu sana.Siyo kila tuhuma ya jinai basi mtuhumiwa ni lazima awekwe ndani mahabusu. It depends.
Huelewi hata maana ya due process, mtu anapotuhumiwa jambo lolote kitu cha kwana polisi wanachotakiwa kufanya ni kupima kwanza kama tuhuma zenyewe zina mashiko. Kitu cha pili polisi wanatakiwa kufanya ni uchunguzi kabla ya kumkamata mtuhumiwa na baada ya uchunguzi wenyewe kama wameona kuna umuhimu wa kumkamata ni kufuata taratibu zote ikiwemo kumuambia wanamkamata kwa kosa au makosa gani hasa ya kisheria. Sasa kwenye hiyo Kangaroo court ya masaa machache haya yote yalifanyika kwa muda gani??Wewe ndio unatumia akili?Kabla ya Mahakama kuthibitisha kwamba mtu ana hatia au la si lazima kuwe na due process.
Polisi ndio wana kazi ya kuhifadhi watuhumiwa,wakili wa Serikali anapeleka kesi Mahakamani na Mahakama inaamua kama yuko guilty au la.
Unapotuhumiwa kijinai haki yako ya kuwa uraiani inakuwa sio haki tena mpaka upewe dhamana Polisi au Mahakamani baada ya kufikishwa huko
Wisdom is chasing you but you are always faster.
Mbona povu sana mkuu? Na unatumia nguvu nyingi sana kuzungumza. Punguza stress.Nani huyo aliagiza Mahakama isimpe dhamana?Amefikishwa mahakamani lini?Hizi hearsay na vikao vya kahawa ni matatizo makubwa. Get your facts right.Acha kukurupuka na kusikiliza viredio mbai.
Kesi yenyewe ya rushwa ya milioni 1!Tena kwa kuiagiza mahakama isimpe dhamana! Upuuzi mtupu
Ndio ushahidi wa kukurupuka.Soma mada nzima uelewe.Huwezi kuchangia kwa kusoma aya moja ukaelewa.Wacha kukurupuka.Mbona povu sana mkuu? Na unatumia nguvu nyingi sana kuzungumza. Punguza stress.
Mimi nimesoma aya ya kwanza tu ya uzi huu unaojadiliwa.
Hata hivyo hizo redio kubwa zilishatekwa na na propaganda za ccm na huyo Makonda wako, bora hata tusikilize redio mbao tu. Unategemea tuupate ukweli TBC?!
Wananchi wamefanya vizuri, wasikubali kutii amri haramu, tuhuma zipo na iendelee kuchunguzwa. Ila Makonda hana mamlaka ya kuzuia mtu kupewa shamans kwa kosa linalodhaminikaHao wananchi wana haraka ya nini?Anahojiwa hajahukumiwa.Ikiwa hana hatiia kwenye tuhuma hizo za kushiriki kuuza eneo la kijiji na sio rushwa ya milioni 1 ataachiwa.Ikiwa ameshiriki hatua za kisheria zitachukuliwa.
Wananchi hao walikuwepo kwenye mkutano na hakuna aliyepinga tuhuma hizo.
Mtendaji aliulizwa kwanini hakutangazia wananchi mkutano huo na hakuwa na majibu ya kuridhisha.
Kupelekwa Takukuru sio kuhukumiwa.
Ardhi Ardhi Ardhi ndio sababu kubwa ya migogoro kwa Arusha na Moshi...Ardhi ya huko ni MafutaKazi sanaa......Arusha hakupoii...kunawaka moto
Dah umenikumbusha mbali.Huelewe hata maana ya due process, mtu anapotuhumiwa jambo lolote kitu cha kwana polisi wanachotakiwa kufanya ni kupima kwanza kama tuhuma zenyewe zina mashiko. Kitu cha pili polisi wanatakiwa kufanya ni uchunguzi kabla ya kumkamata mtuhumiwa na baada ya uchunguzi wenyewe kama wameona kuna umuhimu wa kumkamata ni kufuata taratibu zote ikiwemo kumuambia wanamkamata kwa kosa au makosa gani hasa ya kisheria. Sasa kwenye hiyo Kangaroo court ya masaa machache haya yote yalifanyika kwa muda gani??
Wanaochukua rushwa kubwa hawatendi kosa ila mil 1 ndiyo kosaSiku chache baada ya RC Makonda kuelekeza TAKUKURU wamweke ndani Mtendaji Kata ya Bwawani na asipewe dhamana kwa tuhuma za kuchukua rushwa milioni moja; wananchi wa kati hiyo zaidi ya mia mbili wamekodi magari na kwenda ofisi za TAKUKURU kushinikiza mtendaji huyo aachiwe huru kwani mafisadi wakiongozwa na madiwani na viongozi wa CCM waliofisadi kata hiyo wameanza kutumia ulaghai kuwakandamiza wananchi
Hebu mwacheni Lucas apumzike. Usiku wa kuamkia leo walikumbwa na tetemeko. Ashukuriwe Mungu hakuna madhara yaliyotokea.Lucas Mwashambwa Chawa njoo huku ujibu hizi tuhuma
Sasa fikira hapo huyo OCCID na polisi wenzake wangekurupuka tu kwa kuzingatia hao wanasiasa na kukutia rumande ina maana ungesota jela miezi yote waliyokuwa wanafanya huo uchunguzi wao kwa sababu hiyo tuhuma yenyewe kwa sheria za Tanzania haina dhamana. Ni mfumo mbaya sana polisi kupewa maelekezo na wanasiasa jinsi ya kufanya kazi zao ikiwemo amri za kukamata watuhumiwa kutoka kwa wanasiasa.Dah umenikumbusha mbali.
Nilliwahi kutengenezewa tuhuma ya kipuuzi sana na wanasiasa kuwa natembea na mwanafunzi nikadokezewa na mmoja (aliyewasaliti wenzake), nikamwambia acha waendelee tu nione watanitiaje hatiani.
OCCID alikuwa akija kufanya upelelezi kimyakimya, huku akiambatana na polisi kata wakianzia kwangu eti wananisalimia, kisha wanazama chimbo kufanya upelelezi wao nikiwa nawachora tu (moyoni najisemea "ngoja mhenyeshwe na wanasiasa kwanza, mkijiridhisha ni upuuzi mtapotea kimyakimya mkidhani sijui kinachowaleta").
Walipogundua ni uhuni upelelezi wao ulijifia kimyakimya. Polisi kata alikuja kunisimulia baadaye kuwa walikuwa wakinipeleleza, nikamwambia nilijua sana tu nikawachora mteseke maana mnawaamini sana ccm.
Siku chache baada ya RC Makonda kuelekeza TAKUKURU wamweke ndani Mtendaji Kata ya Bwawani na asipewe dhamana kwa tuhuma za kuchukua rushwa milioni moja; wananchi wa kati hiyo zaidi ya mia mbili wamekodi magari na kwenda ofisi za TAKUKURU kushinikiza mtendaji huyo aachiwe huru kwani mafisadi wakiongozwa na madiwani na viongozi wa CCM waliofisadi kata hiyo wameanza kutumia ulaghai kuwakandamiza wananchi.
Wananchi wamesema mtendaji huyo alipangiwa kufanya kazi kata hiyo mwaka 2019. Alipoanza kazi mashamba ya kijiji yalikuwa yanatumika na viongozi kulima na kujimilikisha kama ya kwao. Mtendaji aliwanyang'anya mashamba hayo viongozi akiwemo diwani na kuwapa wananchi jambo ambalo viongozi hao wa CCM walichukizwa nalo.
Wakati anapangwa kufanya kazi katika kata hiyo hakuna fedha iliyokuwa inakusanywa kama ushuru kutoka kwenye mali za kata; kwa sasa mashamba yanachangia zaidi ya milioni 30.
Amefanikisha kujenga kituo cha afya na shughuli za maendeleo zinaendelea. Aidha, wakati anaingia wanafunzi walikuwa wanapeleka mahindi na maharage kwa ajili ya chakula ila sasa hivi mtendaji huyo ametenga ekari 20 kwa ajili ya shule na kwa mwaka huu shule imevuna zaidi ya gunia 80 zinazotumika kulisha wanafunzi.
Kuhusu rushwa ya milioni moja inayodaiwa na Mkuu wa Mkoa, wananchi wamesema fedha hizo zilitolewa adharani na hazikuwahi kukabidhiwa kwa mtendaji badala yake zilielekezwa kununua vifaa vya ujenzi na kwamba Makonda alipaswa kuwahoji wananchi kuliko kutoka na taarifa ofisini kwake na kwenda kuwakamata watu wasio na hatia kwa maelekezo ya mafisadi wanaotumia mali za umma kuwaumiza viongozi wenye maono kama mtendaji.
Wananchi hao wameitaka TAKUKURU kufanya kazi kwa utaalamu badala ya kufanya kazi kisiasa. Wamehoji kama kweli kulikuwepo rushwa kwanini TAKUKURU haikuwahi kuchunguza badala yake inapokea maelekezo? Wamehoji kwanini TAKUKURU wameshindwa kufika kijijini kufanya mahojiano na wananchi badala yake wamejazana kumweka mahabusu mtendaji ambaye dhamana ni haki yake?
Mwisho, wananchi wanadai mambo aliyoyafanya mtendaji wa Bwawani yanastahili pongezi na siyo kuadhibiwa kama mkuu wa Mkoa anavyofanya. Kama mkuu wa mkoa ana vyombo alipaswa kubaini mapema kwamba viongozi wa CCM wa kata wanatumia ofisi yake kupambana na watendaji wa serikali wanaowatumikia wananchi kwa haki.
Sasa kama kuna haki ya dhamana iweje Rc atoe amri ya kutopewa dhamana na takukuru ni taasisi huru ?Huoni kama mmeacha kufanya kazi kitaalam na sasa mnatumika kisiasa,Unapotuhumiwa unawekwa mahabusu ili kuzuia usiingilie na kujaribu kuharibu ushahidi lakini inategemea na tuhuma zinazokukabili.Pia usisahau kuna haki ya dhamana kwa tuhuma ambazo unaweza kuwekewa dhamana.