Wananchi wa kata ya Bwawani Arusha waandamana kulazimisha TAKUKURU wamwachie Mtendaji Kata aliyewekwa Ndani na Makonda; wadai RC hasikilizi wananchi

Haki gani hasa huyo Afisa Mtendaji Kata ataipata wakati amewekwa ndani mahabusu?? Kitendo tu Cha kumuweka ndani mahabusu tayari umeingilia haki zake na pia kuvunja haki yake ya kuwa huru uraiani. Je, atalipwa Fidia kwa huwa muda ambao atakuwa yupo kizuizini huko mahabusu???
 
Tuhuma za mtendaji zilitakiwa zianzie kwa wananchi na si ofisini kwa Makonda.
 
Wananchi au wewe ndio unataka
 
Reactions: Tui
Kumuhoji mtu lazima umkamate na kumuweka jela??
Unapotuhumiwa unawekwa mahabusu ili kuzuia usiingilie na kujaribu kuharibu ushahidi lakini inategemea na tuhuma zinazokukabili.Pia usisahau kuna haki ya dhamana kwa tuhuma ambazo unaweza kuwekewa dhamana.
 
Tuhuma za mtendaji zilitakiwa zianzie kwa wananchi na si ofisini kwa Makonda.
Zilianzia kwa wananchi kwenye mkutano wa kutatua kero na sio ofisini kwa Makonda. Get your facts right.Wacha kukurupuka
 
Unapotuhumiwa unawekwa mahabusu ili kuzuia usiingilie na kujaribu kuharibu ushahidi lakini inategemea na tuhuma zinazokukabili.Pia usisahau kuna haki ya dhamana kwa tuhuma ambazo unaweza kuwekewa dhamana.
Sheria za Tanzania zinataka mtu akikamatwa na polisi afikishwe mahakamani ndani ya masaa 48 na mahakama ndio inatakiwa itoe maamuzi kama aendelee kushikiliwa rumande au aachiwe kwa dhamana au bila dhamana, sio mkuu wa mkoa au wilaya na polisi wake wajiamulie tu kumuweka mtu ndani jela kadri wanavyoona wao inafaa.
 
Ndio maana nikasema haya maamuzi ya kuyatoa mbele ya watu tena haraka ni ujinga na sio haki kabisa
Makonda kamuonea bila kuchunguza
Chawa hawa wabaya mno
 
Hiyo assumption yako ni kwamba hana hatia.Well and good.Je kama tuhuma hizo ni za kweli kipi kifanyike?A coin has always two sides.
 
How do you make press conference and you don't know how to express. Haya mambo ya kutoa maamuzi yanahitaji uelewa wa hali ya juu sana na sio kukurupuka
 
Hiyo assumption yako ni kwamba hana hatia.Well and good.Je kama tuhuma hizo ni za kweli kipi kifanyike?The coin has always two sides.
Tumia kichwa chako kufikiria badala ya kubebea meno tu, anayeweza kuthibitisha hizo tuhuma kama ni kweli ni mahakama pekee, kuendelea kumuweka jela kabla mahakama haijazithibitisha ni ukiukwaji mkubwa wa haki yake ya kuwa raia huru uraiani.
 
Zilianzia kwa wananchi kwenye mkutano wa kutatua kero na sio ofisini kwa Makonda. Get your facts right.Wacha kukurupuka
Kama ni hivyo hawa wananchi waliokwenda Takukuru ni wa wapi! Inawezekana wale waliokwenda kwa Makonda walitengenezwa ili wamtie matatani.
 
Hiyo assumption yako ni kwamba hana hatia.Well and good.Je kama tuhuma hizo ni za kweli kipi kifanyike?A coin has always two sides.
Kwani Mahakama zipo ili kufanya kazi gani?
Je, Paul Makonda kama Mkuu wa Mkoa kazi yake ni kuthibitisha tuhuma kwa watu wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali????

Inavyoonekana wewe ni 'mbumbumbu' kama alivyo huyo Makonda wako.
 
Hawa wananchi wapewe maua yao
 
Nchi inashangaza kiongozi atoke huko apelekwe Arusha , bora kuacha wan-Arush watafute kiongozi miongoni mwa jamii zao ndio tatizo mpaka mkurugenzi wa jiji ni mwizi.
 
Fi Fidia muhimu
 
Tumia kichwa chako kufikiria badala ya kubebea meno tu, anayeweza kuthibitisha hizo tuhuma kama ni kweli ni mahakama pekee, kuendelea kumuweka jela kabla mahakama haijazithibitisha ni ukiukwaji mkubwa wa haki yake ya kuwa raia huru uraiani.
Wewe ndio unatumia akili?Kabla ya Mahakama kuthibitisha kwamba mtu ana hatia au la si lazima kuwe na due process.
Polisi ndio wana kazi ya kuhifadhi watuhumiwa,wakili wa Serikali anapeleka kesi Mahakamani na Mahakama inaamua kama yuko guilty au la.
Unapotuhumiwa kijinai haki yako ya kuwa uraiani inakuwa sio haki tena mpaka upewe dhamana Polisi au Mahakamani baada ya kufikishwa huko
Wisdom is chasing you but you are always faster.
 
Siyo kila tuhuma ya jinai basi mtuhumiwa ni lazima awekwe ndani mahabusu. It depends.

Isitoshe, dhamana ni haki yake ya msingi kupewa huyo Afisa aliyetuhumiwa. Hata aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Ditopile Mzuzuli alipewa dhamana na kuachiwa huru licha ya kwamba aliua mtu makusudi (dereva wa daladala) tena mchana kweupe huku abiria wake waliokuwepo kwenye hiyo daladala wakishuhudia alivyokuwa akiuawa huyo dereva.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…