Wananchi wa kata ya Bwawani Arusha waandamana kulazimisha TAKUKURU wamwachie Mtendaji Kata aliyewekwa Ndani na Makonda; wadai RC hasikilizi wananchi

Tena kwa kuiagiza mahakama isimpe dhamana! Upuuzi mtupu
Nani huyo aliagiza Mahakama isimpe dhamana?Amefikishwa mahakamani lini?Hizi hearsay na vikao vya kahawa ni matatizo makubwa. Get your facts right.Acha kukurupuka na kusikiliza viredio mbao.
 
Nchi inashangaza kiongozi atoke huko apelekwe Arusha , bora kuacha wan-Arush watafute kiongozi miongoni mwa jamii zao ndio tatizo mpaka mkurugenzi wa jiji ni mwizi.
Sure.

Hili jambo hata Lissu alilifafanua vizuri sana juzikati.
 
Mwaka ukiisha wengi watakuwa wameumizwa. Elimu hutusaidia kuacha kukurupuka na mihemko ya kutafuta sifa!
 
Huelewi hata maana ya due process, mtu anapotuhumiwa jambo lolote kitu cha kwana polisi wanachotakiwa kufanya ni kupima kwanza kama tuhuma zenyewe zina mashiko. Kitu cha pili polisi wanatakiwa kufanya ni uchunguzi kabla ya kumkamata mtuhumiwa na baada ya uchunguzi wenyewe kama wameona kuna umuhimu wa kumkamata ni kufuata taratibu zote ikiwemo kumuambia wanamkamata kwa kosa au makosa gani hasa ya kisheria. Sasa kwenye hiyo Kangaroo court ya masaa machache haya yote yalifanyika kwa muda gani??
 
Nani huyo aliagiza Mahakama isimpe dhamana?Amefikishwa mahakamani lini?Hizi hearsay na vikao vya kahawa ni matatizo makubwa. Get your facts right.Acha kukurupuka na kusikiliza viredio mbai.
Mbona povu sana mkuu? Na unatumia nguvu nyingi sana kuzungumza. Punguza stress.

Mimi nimesoma aya ya kwanza tu ya uzi huu unaojadiliwa.

Hata hivyo hizo redio kubwa zilishatekwa na na propaganda za ccm na huyo Makonda wako, bora hata tusikilize redio mbao tu. Unategemea tuupate ukweli TBC?!
 
Makonda ni kiongozi anayeamini katika kutumia maguvu. Hajui kufanya rational judgement kabla ya maamuzi. Kiufupi hatumii akili, na hili limeumiza wengi.

Biblia inasema "Mkuu asiye na [akili] huwaonea watu wake"
 
Ndio ushahidi wa kukurupuka.Soma mada nzima uelewe.Huwezi kuchangia kwa kusoma aya moja ukaelewa.Wacha kukurupuka.
Ulishakuja na uamuzi wako bila kujua kinachojadiliwa.Ndio herd thinking hiyo.Ni tatizo kubwa
 
Wananchi wamefanya vizuri, wasikubali kutii amri haramu, tuhuma zipo na iendelee kuchunguzwa. Ila Makonda hana mamlaka ya kuzuia mtu kupewa shamans kwa kosa linalodhaminika
 
Dah umenikumbusha mbali.


Nilliwahi kutengenezewa tuhuma ya kipuuzi sana na wanasiasa kuwa natembea na mwanafunzi nikadokezewa na mmoja (aliyewasaliti wenzake), nikamwambia acha waendelee tu nione watanitiaje hatiani.

OCCID alikuwa akija kufanya upelelezi kimyakimya, huku akiambatana na polisi kata wakianzia kwangu eti wananisalimia, kisha wanazama chimbo kufanya upelelezi wao nikiwa nawachora tu (moyoni najisemea "ngoja mhenyeshwe na wanasiasa kwanza, mkijiridhisha ni upuuzi mtapotea kimyakimya mkidhani sijui kinachowaleta").

Walipogundua ni uhuni upelelezi wao ulijifia kimyakimya. Polisi kata alikuja kunisimulia baadaye kuwa walikuwa wakinipeleleza, nikamwambia nilijua sana tu nikawachora mteseke maana mnawaamini sana ccm.
 
Wanaochukua rushwa kubwa hawatendi kosa ila mil 1 ndiyo kosa
 
Sasa fikira hapo huyo OCCID na polisi wenzake wangekurupuka tu kwa kuzingatia hao wanasiasa na kukutia rumande ina maana ungesota jela miezi yote waliyokuwa wanafanya huo uchunguzi wao kwa sababu hiyo tuhuma yenyewe kwa sheria za Tanzania haina dhamana. Ni mfumo mbaya sana polisi kupewa maelekezo na wanasiasa jinsi ya kufanya kazi zao ikiwemo amri za kukamata watuhumiwa kutoka kwa wanasiasa.
 
Unapotuhumiwa unawekwa mahabusu ili kuzuia usiingilie na kujaribu kuharibu ushahidi lakini inategemea na tuhuma zinazokukabili.Pia usisahau kuna haki ya dhamana kwa tuhuma ambazo unaweza kuwekewa dhamana.
Sasa kama kuna haki ya dhamana iweje Rc atoe amri ya kutopewa dhamana na takukuru ni taasisi huru ?Huoni kama mmeacha kufanya kazi kitaalam na sasa mnatumika kisiasa,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…