Uchaguzi 2020 Wananchi wa Kawe mnafahamu jambo hili?

kudamademede

Member
Joined
Jan 1, 2020
Posts
62
Reaction score
241
Wana jamvi, nawasalimu mchana huu na hongera kwa majukumu ya kulijenga Taifa letu pendwa.

Nimefanikiwa kusoma kitabu cha Halima Mdee mbunge aliyemaliza muda wake wa Jimbo la Kawe kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kitabu chenye title TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA JIMBO LA KAWE 2015-2020, kitabu hiki kimejaa kona nyingi sana na giza nyingi kuanzia mwanzo mpaka mwisho wake. Kuna utekelezaji hewa, fedha zilizoelekezwa hazihakisi kabisa uhalisia wa kile kilichofanyika pamoja na miradi ya kusadikika.

Nina uhakika kabisa mtu aliyemshauri Halima Mdee kuandaa kitabu hicho alijua kuwa hajafanya chochote na ndio njia ya kumuonesha kwa wananchi wamjue tunapoelekea kwenye uchaguzi; asante sana muandaaji na mshauri kwa kutuokoa na kirusi hiki tulichoishi nacho kwa miaka 10.

Kelele nyingi zinazopigwa na Wabunge wa upinzani zinaonekana kuwa za kweli lakini kama utekelezaji ni wa namna hii, basi huenda wapinzani wakawa ni hatari sana kuliko mtu yeyote yule.

Namalizia summary ya kitabu hiki na nitaileta kwenu moja kwa moja

Mzalendo wa Kweli
Kawe-Mikoroshini
 
Hayo uyasemayo n ya kweli Kabsa nilipitia baadhi ya nyaraka hakuna alichokamilisha kila kitu n kinaendelea for 10yrs ameshindwa kutatua matatizo ya kawe halima hafai kabsa kuendelea kushikilia kawe
 
Reactions: UCD
Barabara za makongo juu zote ni vumbi tupu ametekeleza nini hapo zaidi ya kuandika uongo na unafki tu?
Akajipange tena maana safari hii hatutamchagua tena
 
Reactions: UCD
Ilo nakubaliana na wewe kabisa namm nlipitia baadhi ya utekelezaji wake lakini ni mambo ambayo sio ya kweli kabisa anatudanganya sisi watu wa kawe hajui na sisi tunaelewa
 
Reactions: UCD
Nakuunga mkono aiseee, anasema kuna mgogoro ameutatua kule cha simba lakini cha ajabu mgogoro huo bado upo mpaka Leo. Sisi ni wananchi na sio watoto wadogo wakudanganywa na tusielewe.

Tunakataa siasa za kipumbavu.
 
Reactions: UCD
Kwa ufupi halima hawezi kuwaletea wanakawe maendeleo kwa mfano tu Rais Magufuli ndani ya miaka mitano amefanya mengi ambayo yanaonekana sasa huyu miaka 10 lakin hakuna kinachoonekana [emoji849]
 
Hii ni kweli kabisa ndugu mwandishi kwasababu hata mimi nimepitia hasa ktk mapato,matumizi,na fedha iliyo bank ya halmashauri kwa mwaka 2017/18 na 2018/19 hii imajaa uongo kwa kutufanya sisi ni wajinga

Halima anatakiwa kukiri kuwa umetudanganya kuwa umetukosea kwa kutupuuza,na jinsi unavyozidi kuongea kwenye Sera zako ni kuzidi kutuona sisi wajinga.
Bi kidude kalale
 
Sijaona alichokifanya ndani ya hiyo miaka kumi, It's time for Gwajima to take place.
Kawe ya Gwajima yani
 
Leta tujuwe uwongo wake tatizo halima porojo nyingi ,hapa kazi tu maneno apeleke kwake
 
Gwajima atabaki kuwa juu tu wewe katafute kazi ya nyingine ya kufanya.
Wana Kawe hatuna tena imani na wewe.
 
Hicho kijitabu hata mimi nimekipitia kina uongo mwingi sana alafu mbaya zaidi katuletea wanakawe ambao tunajua alicho kifanya na ambacho ajafanya.

Hata kama ni kutafuta kura jamani sema ambayo yanaukweli kwa sababu tunaosoma ni wana kawe na ndio tunaona
ukweli humuweka mtu huru halima anaangaika na mambo yote hayo kwa sababu ya uongoo

Na sisi wanakawe hatutaki tena kufanya makosaaa
Tunakwenda na Gwajima
 
Halima Mdee ni mwizi kabisa, barabara zilizokamilika ni zip?
Hakuna barabara hata moja iliyokamilika mwongo mmoja anajaza tu tumbo lake yan anatokea wakati wa kuomba kura tu akipata anapotea Mazimq but not this time wanakawe hatutampa kura zetu tenaaaa
 
Yani tumewashtukia aisee wanatudanganya ili tuendelee kuwapa kura zetu awamu hii tumeamka hawatatupata tena miaka kumi hakuna utekelezaji uliofanyika
 
Watanzania wote wanajua kuwa Magufuli hapeleki pesa kwa Majimbo ya wapinzani ....!!
Kama ni kweli mbona hajasema bungeni wala huwa hateteagi jimbo lake kama kwel ana mapenzi na kawe tuleteenii ushahidi unaonyesha alivyokuwa anapigania jimbo la kawe bungeni na hakupewa pesaa mpaka leo[emoji57]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…