kudamademede
Member
- Jan 1, 2020
- 62
- 241
Wana jamvi, nawasalimu mchana huu na hongera kwa majukumu ya kulijenga Taifa letu pendwa.
Nimefanikiwa kusoma kitabu cha Halima Mdee mbunge aliyemaliza muda wake wa Jimbo la Kawe kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Kitabu chenye title TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA JIMBO LA KAWE 2015-2020, kitabu hiki kimejaa kona nyingi sana na giza nyingi kuanzia mwanzo mpaka mwisho wake. Kuna utekelezaji hewa, fedha zilizoelekezwa hazihakisi kabisa uhalisia wa kile kilichofanyika pamoja na miradi ya kusadikika.
Nina uhakika kabisa mtu aliyemshauri Halima Mdee kuandaa kitabu hicho alijua kuwa hajafanya chochote na ndio njia ya kumuonesha kwa wananchi wamjue tunapoelekea kwenye uchaguzi; asante sana muandaaji na mshauri kwa kutuokoa na kirusi hiki tulichoishi nacho kwa miaka 10.
Kelele nyingi zinazopigwa na Wabunge wa upinzani zinaonekana kuwa za kweli lakini kama utekelezaji ni wa namna hii, basi huenda wapinzani wakawa ni hatari sana kuliko mtu yeyote yule.
Namalizia summary ya kitabu hiki na nitaileta kwenu moja kwa moja
Mzalendo wa Kweli
Kawe-Mikoroshini