Umeligundua hilo mkuu! Nimepoteza muda kuangalia historia za wachangiaji washambulizi. Wote nilio angalia ni members walio jiunga Juni-sept 2020. Why?
Hayo ndiyo yale ya kule Twitter ambako timu ya Gwajiboy ilivamia na slogan ya "tuinuane" ili wakianza kumtetea MTU wao wasomeke na wengi, wakashtukia na kula block za kutosha sasa bado JF.
Labda tujiulize Gwajiboy na watu wake mbona wamejipanga muda mrefu kuingia bungeni kupitia Kawe kwa kutumia mbinu chafu?
Aina ya mbunge kama Halima ni very rare kupatikana hivyo ni bahati kwa Kawe kuwa naye. Halima hata kama Lissu atashinda urais ikifika suala la serikali kuonea wananchi lazima watazinguana tuu maana hana unafiki wala tabia ya kusema NDIYOOO penye HAPANA.
Kuna mambo Halima anaweza kuwa kashindwa kutekeleza Kawe, lakini wananchi tunajuwa kuwa alikuwa anapambana na serikali ya aina gain hasa ambayo iko radhi kuumiza wananchi kwa sababu haimpendi mbunge wa eneo hilo.
Ni wajibu kuiadhibu serikali ya chama hicho kwa kuitoa madarakani kuliko kuipigia magoti tena miaka mitano kwa sababu yenyewe imetupigia magoti kwa siku moja.
View attachment 1586342View attachment 1586343