Uchaguzi 2020 Wananchi wa Kijiji cha Mpeta, Tarafa ya Nguruka, Wilayani Uvinza, Kigoma wasimamisha msafara wa Bi. Hamida Abdallah Huweishi

Uchaguzi 2020 Wananchi wa Kijiji cha Mpeta, Tarafa ya Nguruka, Wilayani Uvinza, Kigoma wasimamisha msafara wa Bi. Hamida Abdallah Huweishi

CUF Habari

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2019
Posts
239
Reaction score
234
Screenshot_20200919-155531.png
WANANCHI WA KIJIJI CHA MPETA TARAFA YA NGURUKA WILAYANI UVINZA MKOANI KIGOMA WAMESIMAMISHA MSAFARA WA MAKAMU WA RAIS, BI. HAMIDA ABDALLAH HUWEISHI NA KUELEZA CHANGAMOTO ZAO KATIKA TARAFA YA NGURUKA.

IMG_20200919_175118_608.jpg

TUSIFANYE MAKOSA IFIKAPO OCTOBA 28,2020 TUMCHAGUE PROF.LIPUMBA AWE RAIS WA NCHI HII TUPATE HUDUMA BORA YA AFYA NA KUDHIBITI VIFO VYA WAJAWAZITO NA WATOTO. "BI HAMIDA ABDALLAH HUWEISHI MAKAMU WA RAIS CUF"

Tutahakikisha kuwa Bajeti ya Wizara ya Afya inapanda na kufikia asilimia 15 ya Bajeti ndani ya miaka 10 ijayo.

Ongezeko la bajeti litawezesha katika kuandaa miundombinu ya kisasa, wataalam, vifaa tiba na vipimo vya kutosha kwa
maradhi yote.

Aidha ongezeko la bajeti litawezesha kutenga fungu maalum kwa ajili ya kukabili maradhi ya milipuko kama COVID-19 kwa kadri
yatakavyojitokeza.

Ili kuhakikisha kuwa kila raia ana haki na anapata huduma za msingi za Afya, Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itahakikisha asilimia 70 ya Watanzania wote wana Bima ya Afya ifikapo 2025 na asilimia 100 ifikapo 2028.

Hatua maalumu zitachukuliwa kuhakikisha kuwa huduma za uzazi bila malipo zinapatikana kwa kila mama mjamzito ili kupunguza vifo vingi vinavyotokea ambavyo vinadhibitika.
 
Hapo ni home! Ni wanafiki hatari, hata shetani akipita huwa tunamsimamisha ili tumuone tumjue..
 
Huyu mama ana uhusiano gani na shetan?? Mbona kama mapacha ivii😇
 
Back
Top Bottom