Pre GE2025 Wananchi wa Kilimanjaro wachangishana kurekebisha barabara mbovu yenye urefu wa kilomita 72

Pre GE2025 Wananchi wa Kilimanjaro wachangishana kurekebisha barabara mbovu yenye urefu wa kilomita 72

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949

Changamoto ya ubovu wa miundombinu ya barabara katika eneo la Kiruweni, Kata ya Mwika Kusini, Wilaya ya Moshi, imewalazimu wananchi wa eneo hilo waishio maeneo mbalimbali nchini kuchangishana fedha na kuanza ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 72 kwa kiwango cha changarawe.

Eneo hilo ambalo wananchi wake wanajishughulisha na uzalishaji wa ndizi na kilimo cha mazao mbalimbali, limekuwa na changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara.

Hali hii imewalazimisha kusafirisha mizigo kwa kichwa hadi sokoni, hivyo kushindwa kufikia ndoto zao za kujikwamua kiuchumi.

Chimbuko la wazo la ujenzi wa barabara lilianzia katika Usharika wa Kiruweni wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), baada ya mvua kubwa zilizonyesha mwishoni mwa Machi na Aprili, 2024.

Mvua hizo zimesababisha barabara hizo zishindwe kupitika kwa vyombo vya usafiri, zikiwamo pikipiki.

Akizungumza kuhusu ujenzi huo, Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kiruweni, Joram Mamuya amesema barabara hizo zimefikia hatua mbaya na kufanya wananchi kushindwa kutumia vyombo vya usafiri na hivyo kulazimika kubeba mazao yao kichwani kuyapeleka sokoni, huku wakitembea umbali mrefu.
 
barabarapic.jpg

Shughuli ya kupanua moja ya barabara zilizoko Kijiji cha Kiruweni Wilaya ya Moshi, ambazo zinajengwa kwa nguvu za wananchi wa eneo hilo ikiendelea ili waweze kuondokana na adha ya kusafirisha mazao kichwani.

Changamoto ya ubovu wa miundombinu ya barabara katika eneo la Kiruweni, Kata ya Mwika Kusini, Wilaya ya Moshi, imewalazimu wananchi wa eneo hilo waishio maeneo mbalimbali nchini kuchangishana fedha na kuanza ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 72 kwa kiwango cha changarawe.

Eneo hilo ambalo wananchi wake wanajishughulisha na uzalishaji wa ndizi na kilimo cha mazao mbalimbali, limekuwa na changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara.
Hali hii imewalazimisha kusafirisha mizigo kwa kichwa hadi sokoni, hivyo kushindwa kufikia ndoto zao za kujikwamua kiuchumi.

Chimbuko la wazo la ujenzi wa barabara lilianzia katika Usharika wa Kiruweni wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), baada ya mvua kubwa zilizonyesha mwishoni mwa Machi na Aprili, 2024.​

barabara2.jpg

Mtambo wa kushindilia barabara ukiendelea na kazi ya kushindilia moja ya barabara katika kijiji cha Kiruweni, Wilaya ya Moshi,mkoani Kilimanjaro, ambazo zinajengwa kwa nguvu za wananchi.

Akizungumza kuhusu ujenzi huo, Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kiruweni, Joram Mamuya amesema barabara hizo zimefikia hatua mbaya na kufanya wananchi kushindwa kutumia vyombo vya usafiri na hivyo kulazimika kubeba mazao yao kichwani kuyapeleka sokoni, huku wakitembea umbali mrefu.

"Barabara zetu zilikuwa zimefikia hatua mbaya na hazikuwa zinapitika. Mwaka huu mvua zilinyesha nyingi, barabara zimeharibika zaidi kiasi kwamba hata wananchi wanashindwa kupeleka ndizi sokoni," amesema Mchungaji Mamuya na kuongeza:
Aidha, amesema kufuatia hali hiyo walilazimika kuwatangazia waamini na wananchi kwa ujumla kuona ni namna gani kutengeneza barabara hizo, ili kurahisisha shughuli za usafiri na kuchochea ukuaji wa uchumi wa eneo hilo.

"Tunamshukuru Mungu, wananchi wetu wanaoishi nje ya hapa waliokuja kusherekea Sikukuu ya Pasaka, ambao walikuwa ibadani siku hiyo, nao waliona changamoto hiyo na wakaamua kuchangia. Aprili 7, 2024 tulianza kuchangia kanisani na kuhamasisha kazi hiyo.

"Tuliwaomba Tarura wakafika, wakakagua barabara na kutupa ushauri namna bora ya kuzifanyia kazi. Sisi kwa pamoja tukaona tuanzie hapo. Gharama walizotupa zilikuwa kubwa, zaidi ya Sh180 milioni, lakini haikutukatisha tamaa. Tuliungana kwa pamoja kama jamii na kuanza kazi hii,” amesema mchungaji huyo.

barabara3.jpg

Mtambo wa kumwagilia maji barabara ukiendelea na kazi hiyo katika moja ya barabara katika kijiji cha Kiruweni, Wilaya ya Moshi,mkoani Kilimanjaro, ambazo zinajengwa kwa nguvu za wananchi.

Wananchi wafunguka
Wakizungumza baadhi ya wananchi wa kijiji hicho, wamesema ujenzi wa barabara hizo utawawezesha kusafirisha mizigo yao kwa urahisi kutoka nyumbani hadi sokoni na kuchochea ukuaji wa uchumi katika eneo hilo.

John Tarimo, amesema barabara hizo walizoea kuzitengeneza kwa majembe ya mkono kupitia msaragambo wa kijiji, lakini kwa sasa hilo lilishindikana kutokana na mvua ambazo ziliharibu zaidi barabara hizo.

Anasema baadhi zilijifunga na nyingine kuwa na mashimo makubwa ambayo yalifanya zisipitike.

"Barabara zetu tumekuwa tukizitengeneza kwa majembe ya mikono na mbaya zaidi kwa sasa kijijini huku hakuna vijana, ni wazee ambao hawawezi kutoka msaragambo kutengeneza barabara, hali iliyosababisha barabara kuharibika na kutopitika kabisa. Hii imechangiwa zaidi na mvua nyingi zilizonyesha mwaka huu,” amesema.
barabara1.jpg

Moja ya barabara zinazoendelea kutengenezwa katika kijiji cha Kiruweni, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro. Picha na Omben Daniel

Tarimo amesema Aprili walivyokwenda kijijini huko, barabara zilikuwa hazipitiki. Kupitia uongozi wa kanisa, wananchi wa eneo hili walijichangisha na kuwashirikisha Wana-Kiruweni wanaoishi maeneo mbalimbali nchini. “Tukashirikishana changamoto hiyo na hivyo tukakubaliana kuchangishana, ili kufungua barabara zote za kijiji hiki ambazo mtandao wake ni kilometa 72,” amesema Tarimo.

Amesema asilimia kubwa ya wakazi wa kijiji hicho ni wakulima, wanahitaji mazao yao yasafirishwe kupeleka sokoni, hali iliyowafanya wengi kuyabeba kichwani kufikia soko kutokana na ubovu wa barabara.

Amesema kutokana na Serikali kukabiliwa na mambo mengi, anatoa wito kwa wananchi katika maeneo mbalimbali kuanza kuchukua hatua ya kutatua changamoto zinazowakabili watu waishio vijijini.
“Tusisubiri kila kitu kifanywe na Serikali. Pale wanapoweza kufanya waunganishe nguvu kama jamii na kufanya jambo, wajitokeze na kufanya. Watu wanapotoka vijijini na kwenda mijini, wakifanikiwa wasisahau nyumbani. Warudi nyumbani kuboresha mazingira ya kwao,” amesisitiza Tarimo.

Shicha Mmbando, mkazi wa kijiji hicho, amesema wameamua kutoa sehemu ya mashamba yao na nguvu kazi, ili kuhakikisha miundombinu ya barabara inapitika kwa urahisi wakati wote wa mvua na kiangazi.

"Barabara zilikuwa ni changamoto. Tunatembea zaidi ya kilometa 10 na mizigo kichwani tukitoa mazao shambani maeneo ya Riata na Holili. Tunapeleka mizigo kichwani kwa sababu magari hayawezi kupita, tunashukuru zikikamilika sasa maisha yatakuwa rahisi," amesema.
 
Shout out to the people in Kiruweni.

You're really setting an example on how to organize and use resources to develop your communities.

I wish we could do the same here in Arusha. It would be great if we could come together as regular citizens raise funds and fix the awful condition of our streets.

Take Njiro Nalopa for instance, the road leading to Elerai is in terrible shape despite being in an area with many wealthy people and government officials. It's really disappointing
 
Safi kabisaa. Hiyo ndio dhana halisi za siasa ya ujamaa na kujitegemea. Naimba mfano huu uchukuliwe kwa watanzania wote, wajue maendeleo watajiletea wenyewee.
Hawalipi Kodi? Yaani Kodu walipe zineende kununua wapinzani, kulipa Bongo Muvi kule Korea then Raia wachangishane kijenga Barabara. Wachaga wamenza ufala
 
Shout out to the people in Kiruweni.

You're really setting an example on how to organize and use resources to develop your communities.

I wish we could do the same here in Arusha. It would be great if we could come together as regular citizens raise funds and fix the awful condition of our streets.

Take Njiro Nalopa for instance, the road leading to Elerai is in terrible shape despite being in an area with many wealthy people and government officials. It's really disappointing
people must stop to pay taxes and use all that money to buils their own roads.
 
Alafu kuna cku mtu atasema tumshukur mh. .... Kuturetea barabara, maan mcc hawakawii
Hizi ndio vitu vinafanya tuonekane maiti, haiwezekani Kodi inakusanywa kila siku ila huduma hazitolewi, wakati huo huo kuna matumizi ya anasa ikiwepo kulipa Bongo move waende korea kufanya ujinga Kununua Magori ya Yanga na Simba. Serikali inagharamaikia Ikulu mbili, Dodoma na Dar.
 
Binafsi napongeza juhudi hizo! Natamani mikoa yote Tanzania iige hivyo.
Hapa sasa Serikali ambacho ingefanya ni kuwaunga mkono kwa kumalizia na rami.
Hapa Dar kama wakazi wangefunguka wakaiga mfano huo kusingekuwa na vilio vya barabara wakati wa mvua!
Waige ufala? huu ni ufala mkubwa mno, pesa za kodi wanaagiza V8 Japani then za kukarabati Barabara hakuna, za kuwalipa Bongo Movie waende Korea zipo ila za Barabara hakuna. Za kugharamaikia kuendesha Ikulu mbili za Dar na Dodoma zipo ila za Barabara hakuna.

Za safari za nje zipo ila za Barabara hakuna.

Huu ni uzuzu yale yale ya kuchangishana kukimbiza ile kibatari.
 
Back
Top Bottom