Pre GE2025 Wananchi wa Kilimanjaro wachangishana kurekebisha barabara mbovu yenye urefu wa kilomita 72

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Aaah umesahau, siyo kabla ya uhuru, ni kabla ya ujio wa Mjerumani.
 
Mkuu watu wanaaminishwa tu chuki dhidi ya mkoa wa K'njaro , hawafanyi hata ka utafiti kadogo

Mtu aliyetengeneza ramani ya barabara ya Mwanga kwenda Milimani Ugweno na Usangi anajulikana.
Mtu huyo hakuwa na certificate lakini alifanya kazi katika serikali upande wa barabara zama hizo wakiitwa ''Com works' yaani common works au CW. Aliombwa na Machifu wa Ugweno na Usangi na akajulikana kama ''Soveya'
Watu hawakujua Soveya ni '' Surveyor'. Ukoo wake upo

Picha za Nyerere akiwa juu ya Land Rover za kueneza TANU Milimani Ugweno na Usangi Zipo na ni kabla ya Uhuru. Mwafrika wa kwanza kupeleka gari anajulikana '' Kajiru'' kama sitakosea kutoka kitabu cha Profesa na ilikuwa miaka ya 1950+

Wataalam wa Baruti na kuvunja miamba koo zao zipo na zinajulikana.

Ukienda Same kule Mbaga kule milimani utashangaa sana jinsi miamba ilivyovunjwa na nguvu ya umma ilivyojenga barabara na miundo mbinu nyingine.

Nimeona dispensary na ipo hadi leo ilijengwa 1905 kwa nguvu za Wananchi.

Zipo shule za Misheni na za Umma zikijulikana kama NA au native authority zipo zimejengwa kabla ya Uhuru

Nimetembea na kuishi sana kuanzi Nanjoka Tunduru hadi Nyakatende Musoma.
Naliendele Mtwara hadi Katoma Kagera.
Pangani Tanga hadi Ujiji Kigoma . Matema Mbeya Beach hadi Ikwiriri Pwani n.k.
Kidogobasi Ifakara hadi Bahi Dodoma. Matombo Morogoro hadi Isevya Tabora.
Ngaranairobi Arusha hadi Mpanda

Nimeona mazuri lakini mabaya pia! Wananchi hawawezi kufyeka barabara wanasubiri serikali

Jamani tuwape MAUA yao wananchi wa K'njaro, tuache wivu, Wazee wao waliwekeza katika Msaragambo

Kinachofanyika Kiruweni katika mada hii ni ''encore'' wao walianza kujiletea maendeleo siku nyingi
 
Kaa apo usubiri kila kitu ufanyiwe na Serikali...Nyie ndio mnaoishi kwa shemeji zenu hadi utu uzima
 
..sidhani kama ni kipindi cha Wajerumani, au kabla ya hapo.
Unafikiri ng'ombe na mbuzi wa;llipita wapi kama hakuna vijia vya kwendea milimani huko.

Mchaga akikwambia barabara miaka 60 nyuma elewa kuwa hicho ni kijia, siyo barabara.
 
Mkuu, kabla hujanijibu kwa kirefu namna hii, unapaswa uelewe tofauti kati ya tozo na kodi. Mimi nimeongelea tozo, wewe unaongelea mambo yanayofanywa na kodi.

Sasa kwa kiingereeza, tozo ni levy, wakati kodi ni tax. Hivi ni vitu viwili tofauti, na sheria za nchi yeyote zinasema hupaswi kutoza kodi ya kitu kile kile mara mbili. Kwa taarifa yako, ili kutovunja sheria, serikali ya CCM huwa inatoza watu kodi na tozo, na kusema hawavunji sheria! Kwa mfano ukinunua umeme Luku au airtime, unalipa kodi (VAT) na tozo (levy), halafu serikali inasema hatukutozi kodi mara mbili, na kodi yetu sio kubwa, huku wakijua wamei break mara mbili ili isionekane kubwa. Ni uongozi wa nchi wanaojua wananchi wake ni mbumbumbu ndio wanafanya vitu kama hivi na wananchi hawaji juu dhidi ya serikali kama wanavyofanya Kenya!

Tozo huwa zina makusudi na matumizi maalum, na zinafanyiwa kitu kinaitwa "ring-fencing". Kwa mfano, tozo kwenye LUKU (REA levy) inatakiwa ikaeneze umeme vijijini lakini serikali haipeleki hizo fedha huko. Tozo kwenye bei ya mafuta (road maintanance levy) inatakiwa itumike kurekebisha barabara na kuhakikisha hakuna mashimo barabarani lakini serikali haipeleki hizo fedha huko wanampa Mwigulu anunue ma-VX ya wake wa maraisi wastaafu kila baada ya miaka mitano sijui, au kupeana posho zisizo na mshiko.

Sasa tozo za miamala ya fedha na simu ni kitu ambacho Samia kwa maneno yake mwenyewe alisema kitatumika kwa ajili ya zahanati na barabara vijijini. Na walipokuja kugundua tozo ziliingiza serikalini fedha nyingi sana kuliko walivyotarajia, wakaamua basi fedha za tozo ziingie kwenye matumizi ambayo yanapaswa kubebwa na kodi, na mengine ambayo sidhani hata kama yanapitishwa na Bunge. Na pia nina wasiwasi kama tozo zinahesabika kama sehemu ya makusanyo ya serikali ambayo yanapangiwa bajeti na Bunge. Tozo mara nyingi ndio fedha zinaliwa sana na viongozi mafisadi.

Ndio maana nikasema, kama tuliambiwa tukubali tozo ili zijenge barabara vijijini na zahanati, na ikaonekana fedha za tozo ni nyingi sana zaidi ya ilivyotarajiwa, kwa nini tuendelee kujitolea fedha kwa ajili ya vitu hivi? Hizo fedha za tozo siku hizi zinapelekwa wapi?
 
Nimekudadafulia namna tozo zinavyotumikaaaa. Bado kitu gani hujaelewaaa
 
Nimekudadafulia namna tozo zinavyotumikaaaa. Bado kitu gani hujaelewaaa
Bado huelewi tofauti ya kodi na tozo. Rudia kusoma nime edit

Haya hapa chini si matumizi ya tozo, ni matumizi ya kodi. Hapo ndipo unapokosea

1. Ujenzi wa barabara kiwango cha rami - inatumika kodi sio tozo
2. Kupeleka fedha shuleni kulipia elimu kuanzia primary hadi advance - inatumika kodi sio tozo
3. Kujenga hospitali na kununua vifaaa tiba na kutoa mishahara na motisha mbalimbali kwa watumishi wa kada ya afya, elimu, ulinzi na usalama n.k inatumika kodi sio tozo
4. Kununua zana za ulinzi na kulipa mishahara na motisha kwa watumishi wa eneo hilo - inatumika kodi sio tozo
5. Kutoa ajira na kupandisha madaraja kwa watumishi wapya na walioko kazi - inatumika kodi sio tozo
 

INASIKITISHA WALLAH.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…