Pre GE2025 Wananchi wa Kilimanjaro wachangishana kurekebisha barabara mbovu yenye urefu wa kilomita 72

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkoa wa kwanza Tanzania kupata lami ni dar es salam unaofuati ni kilimanjaro 1960 na harakati za wanakimanjaro kujipambania zilianza zaman mno kipindi cha KNCU 1933
Waambie ukweli Hawa machawa hawaelewi kitu chochote kabisa!
 
..asilimia 60% ya mkoa wa Kilimanjaro ni wilaya za Same na Mwanga. Je, hali ya maeneo hayo kimiundombinu ikoje?
 
Hizo ni Barabara za kwenda kwenye Mageti ya kupandia mlima. Barabara nyingi moshi vijijini ni mbovu sana hata hizo zilizopo hazikarabatiwi zina mashimo na viraka kila mahali na ni low quality bila hata sidewalks.
Huko kibosho ulipotaja lami inaishia kNCU pale huko kwingine ni mavumbi na matope wakati wa mvua.

Kimsingi Kilimanjaro kama mkoa inahitaji bajeti kubwa kutengeneza Barabara zake. At least zifikie ile level ya Barabara za Kigoma mjini ya sasa au zile za Rwanda.
 
..asilimia 60% ya mkoa wa Kilimanjaro ni wilaya za Same na Mwanga. Je, hali ya maeneo hayo kimiundombinu ikoje?
Same na mwanga nimeenda tu usangi apana tofauti kubwa na maeneo niliyotaja huko kwingine sijafika bado.
 
Safi kabisaa. Hiyo ndio dhana halisi za siasa ya ujamaa na kujitegemea. Naimba mfano huu uchukuliwe kwa watanzania wote, wajue maendeleo watajiletea wenyewee.
Sipingi kuchanga na kujifanyia mambo. Lakini, si huwa wanasema wanatutoza tozo ili ziende barabara vijijini? Sasa kwa nini kuwe na tozo na bado watu wajitolee kuchanga? Nitachukulia hela ya tozo inatumika tofauti na tunavyoambiwa, sivyo?
 
Umenena vizuri mno , ila mimi nimetembea tanzania karibu 50% ndani ndani , kwa asilimia kubwa kilimanjaro na baadhi ya mikoa barabara zake zina nafuu kiasi fulani.
 
Same na mwanga nimeenda tu usangi apana tofauti kubwa na maeneo niliyotaja huko kwingine sijafika bado.

..miundombinu ya Uchagani ilijengwa wakati wa ukoloni wa Muingereza.

..according to Joseph Selasini, Marangu walichagua barabara. Rombo walichagua maji. Sikumbuki alisema maeneo mengine walichagua mradi gani.

..ukisoma michango ya hapa JF kuna mashambulizi mabaya dhidi ya watu wa Kilimanjaro kwamba serikali za baada ya uhuru ziliwapendelea. Ni kama kuna mkakati mahsusi umesukwa dhidi ya Kilimanjaro.

..mazingira hayo ndio yamenifanya nikukumbushe kwamba kuna 60% ya mkoa wa Kilimanjaro, kwa maana ya wilaya za Same, na Mwanga, ambako hali ya miundombinu ni mbaya.

..Na habari ya wananchi wa Kilimanjaro kujitolea kujenga barabara sio ngeni. Walifanya hivyo kabla ya uhuru, na baada ya uhuru.
 
Hili jambo lina ukweli fulani ila mimi naona ili kubalance keki ya taifa ni bora kuwe na majimbo ambayo yatajisimamia yenyewe kwenye maendeleo huku serikali kuu ikitoa support tu.
 
Sipingi kuchanga na kujifanyia mambo. Lakini, si huwa wanasema wanatutoza tozo ili ziende barabara vijijini? Sasa kwa nini kuwe na tozo na bado watu wajitolee kuchanga? Nitachukulia hela ya tozo inatumika tofauti na tunavyoambiwa, sivyo?
Tozo yako na kodi yako, inafanya mambo mengi ambayo kwa namna moja au nyingine wanainchi wanaila kwenye maeneo kama vile
1. Ujenzi wa barabara kiwango cha rami
2. Kupeleka fedha shuleni kulipia elimu kuanzia primary hadi advance
3. Kujenga vituo vya afya , zahanati, na hospitali na kununua vifaaa tiba na kutoa mishahara na motisha mbalimbali kwa watumishi wa kada ya afya, elimu, ulinzi na usalama n.k
4. Kununua zana za ulinzi na kulipa mishahara na motisha kwa watumishi wa eneo hilo.
5. Kutoa ajira na kupandisha madaraja kwa watumishi wapya na walioko kazini.

Hivyo jamaa yanguuu kodi na tozo tunazotozwa ni raia wenyewe ndio wanufaika kwa sehemu ya matumizi kama nilivyoorodhesha apo juuu.
Hivyo kwa mkutadha huo ni vyema wananchi kama hao walioamua kujenga barabara kwa nguvu zao, hiii ndio ujamaa na kujitegemea.
 
Acha ujinga wewe!
 
Hili jambo lina ukweli fulani ila mimi naona ili kubalance keki ya taifa ni bora kuwe na majimbo ambayo yatajisimamia yenyewe kwenye maendeleo huku serikali kuu ikitoa support tu.

..kuna watu hapa JF wana CHUKI na huo mkoa wangekuwa na uwezo wangeupiga mabomu, au kuutia kibiriti.

..lakini kama nilivyokwambia kuna maeneo yana miundombinu mibovu kuliko hata walikotoka hao waliofundishwa kuichukia Kilimanjaro.
 
Mkoa wa kwanza Tanzania kupata lami ni dar es salam unaofuati ni kilimanjaro 1960 na harakati za wanakimanjaro kujipambania zilianza zaman mno kipindi cha KNCU 1933
Hapana, mkoa wa kwanza Tanganyika kupata lami ulikuwa Tanga.

Hiyo yote ni historia, cha muhimu hao wanakijiji siyo wao wa kwanza kuanza kujenga barabara kwa kujitolea wenyewe. Wamechelewa usingizini, lakini tunawapa hongera, mikoa mingine bado wamelala.
 
Hiyo yote ni mikoa ya mwanzo kabisa kupata lami baada ya uhuru nakubaliana na wewe kabisa.
 
..kuna watu hapa JF wana CHUKI na huo mkoa wangekuwa na uwezo wangeupiga mabomu, au kuutia kibiriti.

..lakini kama nilivyokwambia kuna maeneo yana miundombinu mibovu kuliko hata walikotoka hao waliofundishwa kuichukia Kilimanjaro.
😁Sikuwahi kulijua hilo ,ila mbona naona watu wa kutokea huko wanamaelewano mazuri tu na jamii nyingne, na watu wa huko wengi wamesambaa maeneo mbalimbali tu?
 
Safi.
 
kama isingekuwa nyerere, mareale angekuwa ametufikisha mbali sana, sasaivi tungekuwa na nchi yetu. wachaga siku zote tupo serious na maendeleo.
 
Safi kabisaa. Hiyo ndio dhana halisi za siasa ya ujamaa na kujitegemea. Naimba mfano huu uchukuliwe kwa watanzania wote, wajue maendeleo watajiletea wenyewee.
Ujamaa gani wakati hao ni capitalists wenye biashara kubwa? Ingekua ujamaa wasingekuwa na fedha ya kujenga barabara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…