LGE2024 Wananchi wa Lupembe wako tayari kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa

LGE2024 Wananchi wa Lupembe wako tayari kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wananchi wa jimbo la Lupembe wameeleza utayari wao kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika leo Novemba 27, 2024 Nchi nzima huku wakiweka wazi Matarajio yao kwa viongozi wapya watakaochaguliwa

Wananchi hao akiwemo Fikiria Vicent Kisogole, Salvina Barton Mpolo na Martina Isdol Hongoli wamesema hayo jana wakati wa kuhitimisha kampeni za wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika kijiji hicho wakisema uongozi mpya utakaochaguliwa leo uzingatie mahitaji ya wananchi ikiwemo kumalizia miradi ya kimaendeleo ndani ya kijiji hicho.
1732632443351.png
Katika hatua nyingine wananchi hao wameomba uongozi mpya utakaochaguliwa kuhakikisha wanafatilia upatikanaji wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan ili iwafikie huku wanawake wakieleza mahitaji yao kwa uongozi wapya.

Akizungumza katika kampeni hizo Diwani wa kata jirani ya Ukalawa Javani Daniel amewaomba wankanikelele kujitokeza kwa wingi kuwachagua viongozi wa chama cha mapinduzi CCM kwani Chini ya uongozi wa chama hicho mpaka sasa iko miradi mingi ambayo imefanyika na kukamilika katika kata ya ukalawa na kijiji cha kanikelele.
1732632498331.png
Akinadi sera zake Mgombea wa nafasi ya uenyekiti kijiji cha Kanikele kupitia chama cha Mapinduzi ccm Michael Biton Mgeta amesema kwa kuwa toka kampeni zimeanza ameahidi mengi na kilichbakia ni utekelezaji akatumia nafasi hiyo kuomba kupigiwa kura pamoja na wajumbe anaogombea nao kupitia chama chake cha CCM

Nae Mbunge wa Jimbo la Lupembe Edwin Enosy Swale katika kuhitimisha kampeni hizo akiwa Kijiji cha Kanikelele amesema wananchi wa Kijiji hicho wanapaswa kuchukua uamuzi sahihi wa kuwachagua viongozi waliogombea kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi ccm ili kurahisisha ushirikiano kati yake na viongozi wa chini yake huku akigusia miradi ya kimaendeleo iliyotekelezwa katika kijiji hicho.
1732632427373.png
 
Back
Top Bottom