Wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro wamemshukuru Rais Magufuli kwa kuwarejeshea usafiri wa treni kwa nauli nafuu ya sh 16,000 tu

Wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro wamemshukuru Rais Magufuli kwa kuwarejeshea usafiri wa treni kwa nauli nafuu ya sh 16,000 tu

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro wameishukuru serikali ya awamu ya 5 hususani mh Rais Magufuli kwa kuwarejeshea Huduma ya usafiri wa treni uliosimama kwa zaidi ya miaka 20.

Wananchi hao wamesema sasa wana uhakika wa kwenda kula Krismas na mwaka mpya huko Moshi kwa sababu NAULI ya sh 16,000 kwa safari ni rafiki.

Wananchi hao wameishukuru pia CCM kwa kuhakikisha Ilani ya uchaguzi inatekelezwa kwa 100% mkoani Kilimanjaro.

Naye mwenezi wa CCM ndugu Polepole amewaahidi wakazi hao wa Kilimanjaro kuwa CCM itaendelea kuwafanyia mambo makubwa zaidi kama wataendelea kutoa ushirikiano kama wanavyofanya sasa.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Hakuna mwenyeji wa Kilimanjaro anayeweza kushabikia huo uchafu wewe,ni kwamba mumewachukua walevi mukawaweka kwenye camera ili kutuzuga.

Mchagga aache kupanda private car from Dar to Moshi aashobokee hayo matakataka yenu..???
Eti wamepata uhakika wa kwenda Moshi kula Xmas mwaka huu...kwani walikuwa hawana uhakika..???mnachekesha walionuna nyie mafala.

Kilimanjaro imeendelea kabla ya Uhuru kwa taarifa yenu sasa.
 
Acha unafik !
Umesikia kwa nani?.
Piga simu usikie majibu.
Kampeni za kijinga.
Nauli inazidi mpaka basi na unasafiri usiku kucha..kwenda Moshi tu kama kwenda Kigoma?
Nasikia nafasi zimejaa mapaka mwezi wa tatu mwakani..dah[emoji577][emoji920][emoji920][emoji920][emoji920][emoji920][emoji920][emoji920][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hapandi mtu, Nani anapanda gogo linafika Moshi baada ya siku 2 au 3? Wachagga sio masikini hivyo!

Hizi train zita prove failure on the arrival! Hapandi mtu nakwambia! Mtu anataka apakie afike Moshi siku hiyo hiyo! Hizo treni zitapakia ndizi na nguruwe kutoka Moshi kuja Dar!

Believe me!
Hapakii mtu mle!
 
Hakuna mchaga analiye na lafudhi uliyoiandika hapa, tena uache upang'ang'a.
Mimi ni mchaga bro, wa Marangu namkubali sana JPM kuliko huyu kaka yangu muhuni muhuni tu maendeleo hayana chama wahuni wanatuchafua.
 
Hakuna mwenyeji wa Kilimanjaro anayeweza kushabikia huo uchafu wewe,ni kwamba mumewachukua walevi mukawaweka kwenye camera ili kutuzuga.

Mchagga aache kupanda private car from Dar to Moshi aashobokee hayo matakataka yenu..???
Eti wamepata uhakika wa kwenda Moshi kula Xmas mwaka huu...fyuuuuuuuu....kwani walikuwa hawana uhakika..???mnachekesha walionuna nyie mafala.

Kilimanjaro imeendelea kabla ya Uhuru kwa taarifa yenu sasa.
Acha uzwazwa kwa hiyo wachaga wore wanamiliki magari au wote wanamudu gharama za kutumia usafiri binafsi?
 
Back
Top Bottom