Katika hali ya kawaida, ungetegemea wananchi kutokuunga mkono mapinduzi dhidi ya viongozi wao waliowachagua wenyewe!! Tatizo ni kwamba baada ya kuchaguliwa viongozi huamua kuwa vibaraka wa mabeberu wa nchi za magharibi na kuwasahau wananchi waliowaweka madarakani! Sasa Rais aliyepinduliwa badala ya kutetewa na wananchi wake, anatetewa na mabeberu wa magharibi!! Ni aibu!!
Hii inatakiwa kuwa wake-up call kwa viongozi wote wa Africa walioamua kuweka vichwa vyao kwenye Vyungu wakaacha wananchi wao kwenye lindi la Umasikini
Urithi wa Taifa unagawanywa Bure kwa Mzungu halafu mzawa na makodi kibao kwenye kila kitu anachofanya
Hata biashara, Unatozwa kodi kwa wazo tuu kabla hujalijaribu kama litakutoa
Tujifunze kwa Niger
Wazungu wanatutisha kuwa sisi sio kitu bila wao kumbe wao ndio sio lolote bila sisi Angalia France alivyofukuzwa Niger na west Africa in general anavyolia
Viongozi wetu waanze kuandaa Mikataba ambayo itadai 50/50 ya kile ambacho mzungu ana kihitaji zaidi toka kwetu
Sio anakuja anachukua makaa ya mawe
Gas , Madini Aina zote mpaka wanyama anatajirisha kwao halafu anakukopesha pesa Ile Ile ambayo alitakiwa kukupa kama share
Ukiwa Kwao watoto wao wanakuambia"rudini kwenu Africa dark continent" kumbe wao ndio walitakiwa kuondoka kwetu
Wanasahau kuwa Wakati wao wakila nyama mbichi na kuishi mapangoni, Africa tulisha Gundua moto na kuanza kula vya kupikwa Na Mataifa Tajiri kama Mali Etc au turudie kusoma Habari za Timbuktu, Mansa Musa Kan Kan, Biashara za Sofala nk
West Africa ndio Eneo pekee limekuwa la moto miaka yote naona Ile Arab springs ikija ukanda huu
Kitu ambacho Mkoloni wa Leo alijisahau ni kuwa waasisi wa mapinduzi haya wamepita kwenye vikosi vyao high level training
Hata Idd Amin
Kiongozi yeyote asie Jali masilahi ya Raia wake Hana haja ya kusalia madarakani anatakiwa kuondoka kwa njia yeyote Ile.
Mapinduzi ndio uelekeo wa sasa
Rais Utimize ahadi, Boresha maisha ya watu wako au Uondolewe.