Kuchukua nchi kijeshi sio suluhu maana mwisho wa siku hata jeshi lenyewe linaongozwa na wachumia tumbo, fuatilia kwa makini viongozi waandamizi jeshini, wakiingizwa mfukoni kwa tamaa zao yanakua yake yale na tatizo hauwezi ukawakosoa.
Kimsingi ni kusisitiza utawala wa sheria na uwajibishanaji, hakuna beberu huja na kupora kwa nguvu, mnawapa nyie wenyewe kwa tamaa za wachache. Haitokuja niwalaumu hao mabeberu maana hawaibi au kuchukua kwa kutumia mabavu, kuanzia wazungu, Wachina na hata Waarabu hawa hawa mnaosema wanajichukulia bandari zenu, hakuna anayetumia mtutu.
Waafrika tujilaumu wenyewe, hebu angalia hii picha Lagos ilivyokua wakati wa utawala wa mzungu miaka ya 60